Papa Francisko anasema, "Wakati wa kuanza utume kama Papa , nimerudia mara kwa mara kwa namna ya pekee juu ya wasiwasi kutokana na uchungu wa wahamiaji wengi wanaokimbia vita, mateso, majanga ya asili na umaskini. Hizi ni hali za ishara za nyakati, ambazo nimejaribu kutafakari matukio haya nikiomba mwanga wa Roho Mtakatifu tangu nilipotembelea Lampedusa tarehe 8 Julai 2013. Katika kufanya mabadiliko ya Baraza jipya kwa ajili ya Huduma ya Maendeleo endelevu ya binadamu, nilipendelea kwamba sehemu hii ya kijamii iwe chini ya Uongozi wangu , ili kuweza kuhamasisha zaidi Kanisa juu ya wahamiaji , msongamano, wakimbizi na waathirika wa biashara ya binadamu ya binadamu".
Huu ni utangulizi wa Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya Wahamiaji Duniani kwa Mwaka 2018 ulitolewa Jumatatu 21 Agosti 2017. Baba Mtakatifu Francisko anaandika; kila mgeni anaye bisha hodi katika milango yetu, ni fursa ya kukutana na Yesu Kristo, ambaye anajifananisha na mgeni wa kukaribishwa au kukataliwa kila nyakati (Mt 25,35.43).Bwana anawakabidhi upendo wa umama wa Kanisa kila binadamu yoyote anayelazimika kuacha nchi yake akitafuta maisha bora ya baadaye. Wito huo unapaswa kujieleza kwa dhati kila hatua ya uzoefu wa wahamiaji kwa maana ya kuanzia safari hadi kufika na kurudi tena. Ni uwajibu mkubwa ambao Kanisa linataka kushirikisha wote, kwa waamini , wake kwa waume wenye mapenzi mema ambao wameitwa kujibu kwa upendo, hekima, mtazamo mwema , na kila mmoja kadiri ya uwezo wa kila mmoja.
Kwa upande wa suala hili, Baba Mtakatifu anasisitiza kwa kuyaweka katika vipengele vya maneno manne ya mafundisho ya Kanisa yaani kukaribisha , kulinda, kuhamasisha na kushirikisha. Amefafanua kila kipengele akisema; katika kufikiria matukio ya sasa, kukaribisha maana yake hawali ya yote ni kuwezesha wahamiaji na wakimbizi uwezekano mpana wa kuingia kwa usalama na halali katika nchi wanazotamia. Kwa maana hiyo inatakiwa shughuli madhubuti ya kuongeza juhudi katika kuharakisisha ruhusa ya visa ya binadamu ili waweze kuwafikia familia zao. Hata hivyo, Baba Mtakatifu anawaomba kwamba idadi kubwa ya nchi waweze kukubali mipango ya wafadhili(Sponsorship) binafsi na jummuiya za kuweza kufungua mikondo ya kibinadamu kwa ajili ya wakimbizi zaidi walio athirika.Vilevile ingekuwa ni mwafaka kutoa visa ya muda mfupi na hasa kwa watu ambao wanakimbia migogoro katika nchi jirani.
Kuhusiana na suala la kuwarudisha wakimbizi, Baba Mtakatifu anasema siyo suluhisho la kuwarudisha kimkumbo wahamiaji na wakimbizi hasa wale wanaotoka katika nchi ambazo haziweze kuhakikisha heshima na adhi msingi ya binadamu. Kwa njia hiyo anasisitiza umuhimu wa kuwasadia na kuwawezesha wahamiaji na wakimbizi maeneo yanayoridhisha. Mipango ya mapokezi iliyotawanyika katika maeneo tayari mengi anafikiri kwamba inasaidia kwa kiasi fulani makutano binafsi ili kuwawezesha kuwa na hudumazilizo bora na zenye kufaa. Aidha anasisitiza kuwa kiini cha msingi wa Binadamu,kama ilivyoelezwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa XVI inatoa ulazima wa kuweka usalama binafsi na ule wa taifa. Kwa njia hiyo ni lazima kuwapo wataalamu wa uchunguzi katika mipaka.
Hiyo ni kwasababu hali ya wahamiaji wanaotafuta hifadhi na wakimbizi, wanahitaji
uhakika wa usalama wao binafsi na hupatikanaji wa huduma msingi,kwa njia hiyo, kwa
jina la heshima msingi ya kila mtu ni lazima kujitahidi kutafuta njia mbadala kwa
wale wanaoingia katika nchi bila ruhusa.
Kipengele cha pili ni kuhusu kulinda, ni kitendo linachojikita katika aina mbalimbali
za matendo ya ulinzi wa haki na hadhi ya wahamiaji na wakimbizi, bila kujali hali
yao ya kuhamahama. Ulinzi huo huanzia nyumbani kwao, na hasa zaidi uanzie katika utoaji
wa taarifa fulani na kuthibitishwa kabla ya kuondoka kwao, hiyo ni kwasababu ya ulinzi
wao ili kuodokana na ukiukwaji wa sheria ya kuingia bila vibali.Hiyo ingeweza kuendelea
kwa kiasi fulani iwezekanavyo katika nchi ya uhamiaji kwa kuhakikishia wahamiaji
wanapata misaada ya kutosha na kitulizo, haki ya kutunza nyaraka zao na vitambulisho
vyao binafsi,hupatikanaji wa haki sawa, uwezekano wa kufungua akaunti ya benki na
dhamana ya kiwango cha chini cha maisha. Iwapo vitambulisho vyao vina fursa ya kutambuliwa
thamani yake, uwezo na ujuzi wa wahamiaji wanaoomba hifadhi na wakimbizi hawa wanawakilisha
rasilimali kwa jumuiya ambazo zimewapokea.
Kwa njia hyo Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kusema kuwa anayo matumaini ya kwamba kwa heshima na utu wao, wanaweza kupata uhuru wa kwenda katika nchi zinazowapokea, uwezekano wa kufanya kazi na uwezekano wa mawasiliano ya simu. Kwa wale ambao wanaamua kurudi nyumani kwao, Baba Mtakatifu anasisitiza, wapate fursa ya nafasi ya kuendeleza mipango ya kitaalamu na kijamii,aidha kuwaunganisha na jamii. Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto hutoa msingi wa kisheria kwa ajili ya ulinzi wa watoto wahamiaji. Kwa ajili yao ni muhimu kuepuka aina yoyote ya kizuizi kutokana na hali ya kuwa wahamiaji, wakati huo ni lazima kuhakikisha upatikanaji wa shule za msingi na sekondari. Kadhalika ni muhimu kuhakikisha mafunzo ya kudumu nyakati zijazo kulingana na umri wao na uwezekano wa kuendelea na masomo yao. Kwa watoto wanaofika bila kusindikizwa au wametengana na familia zao ni muhimu kuunda mipango ya muda mfupi au kuwakabidhi katika malezi.
Kuhusiana na utaifa wa watoto, Baba Mtakatifu Francisko anaendelea; kwa sababu ya haki kwa wote kwa taifa, wanapaswa kutambuliwa ipasavyo kuthibitishwa na kuandikishwa kwa watoto wote wavulana na wasichana wakati wa kuzaliwa, ili kuweza kepupka kukosa utaifa ambao wakati mwingine wanajikuta wahamiaji na wakimbizi. Inawezekana ki urahisi kuzuiwa kwa njia ya kuandikishwa uraia kwa mujibu wa kanuni za sheria za kimataifa. Hali za wote wanaohama isiwe kizuizi cha upatikanaji wa huduma ya afya na pensheni ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na uhamisho wa michango yao ikitokea kurudishwa makwao.
Kuhamasisha maana yake ni uwezo msingi wa kuhakikisha kwamba wahamiaji wote na wakimbzi kama pia jumuiya ambazo zinawapokea, waweze kuwekwa katika hali inayorodhisha katika kipimo cha ubinadamu aliyependwa na Muumba. Kati ya vipimo hivyo , ni lazima kutoa thamani ya haki na mwelekeo wa kidini, kuhakikisha kwamba wageni wote waliopo katika eneo wanao uhuru wa kukiri imani yao. Wakimbizi na wahamiaji wengi wana ujuzi ambao unapaswa kuthibitishwa na kutolewa thamani yake. Kwa kuwa "kazi ya binadamu, kwa tabia yake ina maana ya kuunganisha watu," Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo wa kufanya kila linalowezekana ili waweze kuhamasisha na kukuza ile hali ya kuwaunganisha kijamii katika kazi wahamiaji na wakimbizi, kuhakikisha ni kwa wote ikiwa ni pamoja na wanaotafuta hifadhi uwezo wa kufanya kazi, mafunzo lugha na kazi ya uraia ya kutosha katika lugha zao za asili.
Kwa upande wa watoto wahamiaji, inahitajika kazi ya kushirikiana kwa pamoja kwa namna ya kuweza kuzuia matumizi mabaya na vitisho na hathari dhidi ya ukuaji wao wa kawaida. Mwaka 2006, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI alionyesha jinsi gani suala ya familia za wahamiaji kuwa ni rasilimali ya utamaduni wa maisha na sababu ya kuunganisha thamani na maadili.Uadilifu wake lazima ukuzwa, kwa kutafuta jinsi ya kuwaunganisha pamoja na familia zao na ndugu zao kama babu na bibi, na ndugu wengine bila kutegemea tu mahitaji ya kiuchumi. Kwa upande wa hali ya wahamiaji na wakimbizi wanaotaka hifadhi katika hali ya ulemavu, lazima kuwalinda na kuwahakikishia zaidi umakini na msaada.Wakati kuzingatia juhudi kubwa hadi sasa za nchi nyingi katika suala la ushirikiano wa kimataifa na misaada ya kibinadamu, Baba mtakatifu Francisko anayo matumaini ya kwamba katika ugawaji wa misaada hiyo itakuwa ni kuzingatia mahitaji (kwa mfano, huduma ya afya, jamii na elimu) ya nchi zinazoendelea ambazo zinapokea mtiririko mkubwa wa wakimbizi na wahamiaji, vivyo hivyo,wanajikuta katika hali mbaya hata wale waliopokea kwa ukosefu wa zana na kuishi katika mazingira magumu.
Neno la mwisho, ni kushirikisha, Baba Mtakatifu Francisko anaeleza juu ya neno hili kuwa, hii inahusiana na fursa ya nafasi ambayo ni utajiri wa utamaduni unaotokana na uwepo wa wahamiaji na wakimbizi.Kushirikishana hauna maana ya kufananishaambao utaka kukandamiza au kusahau utamaduni wao wenyewe au utambulisho. Kumbe kuwasiliana na wengine husababisha kugundua siri ya kuwa wazi na kukaribishana na kupekeana katika masuala mbalimbali na kuchangia uelewa mkubwa wa pamoja. Ni mchakato wa muda mrefu na hivyo una lengo la kuunda sura ya jamii na utamaduni kuwa zawadi ya Mungu kwa watu.Mchakato huu unaweza kuwa wa kasi kwa njia ya kutoa ofa ya uraia usiyo ingiliana na mahitaji ya kiuchumi kama vile lugha na mipango ya mafunzo halali kwa namna ya pekee kwa wahamiaji ambao wanaweza kukaa kwa muda mrefu katika nchi. Kwa namna hiyo Baba Mtakatifu anasisitiza tena muhimu wa kukuza kwa kila njia utamaduni wa kukutana na kuzidisha fursa kwa ajili ya kubadilishana utamaduni, kuhifadhi na kusambaza mbinu bora za ushirikiano na kuendelezamazungumzo na kujiandaa kijamii katika mchakato kamili.
Kwa mujibu wa mila na desturi za uchungaji, Kanisa liko tayari kujikita katika kutekeleza mipango hawali ya yote ya binadamu iliyopendekezwa, lakini ili kuweza kupata matokeo yanayotarajiwa ni muhimu kwamba jamii nzima ya kisaisa na raia wote pamoja kila mmoja kulingana na majukumu yake kujikita barabara katika utekelezaji wa maelekezo hayo. Baba Mtakatifu pia anaeleza; wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa, mjini New York tarehe 19 Septemba, 2016, viongozi wa dunia walionyesha wazi nia yao ya kufanya juhudi kwa ajili ya wahamiaji na wakimbizi na kuokoa maisha yao na kulinda haki zao, kwa kushirikiana wajibu kwa ngazi ya taifa. Hadi sasa nchi wanachama bado wanayo lengo na maandalizi ya kuidhinisha ifikapo mwishoni wa 2018 mikataba miwili ya kimataifa (Global Compacts), moja unahusu wakimbizi na mwingine ni wahamiaji.
Anamalizia akisema, katika mwanga wa taratibu wa michakato hii, miezi michache ijayo itawasilisha fursa nzuri ya kusaidia hatua madhubuti ambayo Baba Mtakatifu amependelea kuitafsiri katika vipengele vinne. Anawaalika kuchukua fursa hiyo kwa kila mtu katika nafasi kushirikisha ujumbe kwa wote, kwa wahusika wa kisiasa na kijamii au wadau katika machakato ambao utafikia kutoa idhini ya mikataba miwili ya kimataifa.
Leo ni tarehe 15 Agosti wakati Kanisa linaadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria kupalizwa
mbinguni. Mama wa Mungu alifanya uzoefu mgumu wa uhamisho(Mt 2,15-15) alimsindikiza
mwanae kwa upendo na hata katika njia ya msalaba,na sasa anshiriki utukufu milele.
Kwa maombezi yake ya kimama, tunamkabidhi matumaini ya wahamiaji na wakimbzi wote
dunaiani na matarajio ya jamii ambayo inawapokea, ili kwamba kwa mujibu wa amri kuu
ya Mungu ,tunaweza wote kujifunza kupenda mgeni kama sisi wenyewe tunavyojipenda.
Vatican, 15 Agosti 2017
Sikukuu ya Bikira Maria Mpalizwa.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |