2017-08-22 14:52:00

Mkutano wa IX wa Familia duniani 2018 kuanza maandalizi mjini Dublin


Hivi karibuni  umefanyika mkutano kuhusu maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya IX ya Familia  Duniani 2018  Jimbo kuu la Dublin, nchini Ireland. Mkutano huo umefanyikia katika madhabahu ya kitaifa ya mama Maria huko Knock. Askofu Mkuu Mkuu Diarmuid Martin pamoja na Padre Timothy Bartlett Katibu Mkuu wa Siku ya IX ya Familia duniani wamewasilisha ratiba ya maandalizi ambayo inatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 21 hadi 26 Agosti 2018 Dublin.Kauli mbiu ya Siku hiyo ya IX ya familia duniani ni “Injili ya familia, furaha kwa Ulimwengu". Tamasha la Kimataifa ambalo lilipendekezwa  na Mtakatifu Yohane Paulo II unaangukia katika mwaka wa tatu ambao kwa dhati utafanyikia  mjini Dublin mwaka 2018. 

Katika barua ya tarehe 25 Machi mwaka huu Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waandaaji na watakao shiriki mkutano huo kutafakari kwa kina juu ya mafundiho ya Wosia wake wa Furaha ya upendo ( Amoris laetitia) ambayo Kanisa linataka familia itembee daima katika hija ya ndani kwa dhihirisho halisi la maisha. Mkurugenzi wa ofisi ya kichungaji kwa ajili ya familia ya Baraza la Maaskofu wa Italia (Cei) Padre Paolo Gentili amekuwa mmojawapo wa kundi la kuandaa mikutano ya kimataifa ameeleza ni jinsi gani ya kuandaa mkutano mkuu kama huo kwamba kwa mara ya kwanza kamati ya maandalizi iliamua kuwaalika makundi mbalimbali kutoka mabaraza yote ya maaskofu duniani.

Mwezi mmoja uliopitia wamekuwa na mkutano ambao waliweza kuishi kindugu , waligawanyika katika makundi kulingana na lugha zao na kuanza kutafakari juu ya mada na hasa kuandaa moyo wa kuweza kupokea familia nyingi ambazo zitapendelea kushiriki.
Hata hivyo wandaaji waliunda program mpya kutoka katika wosia  isemayo “tunaongea juu ya familia na sisi ni familia", lengo lake ni mafunzo yanayo anzia katika wosia wa Furaha ya Upendo ambayo itawasaidia maparokia yote duniani kuanzia kipindi cha hivi karibuni cha Vuli. Mafunzo hayo pia yataoneshwa kwa njia ya video, maandiko na tamasha. Pia  hizi ni shughuli ambazo zitasaidia katika safari ya maandalizi kuelea katika kilele cha 2018 huko Dublin Ireland.

Aidha akielezea juu ya Kanisa la Ireland amesema, katika utafiti inaonesha kuwa Kanisa la Ireland kwa miaka ya hivi karibuni ushiriki umeshuka. Kwa njia hiyo ni Kanisa linalojikita kutafuta pia ambalo linataka kufundisha mbinu mpya ya hali ya maisha ndani ya familia. Padri anasema mara nyingi kuna parokia ambazo zimejiweka katika miundo kama vile mikutano ambayo inafanyika kuhusu mapendekezo ya njia za kufuata, lakini hiyo haitoshi. Ni lazima kuingia ndani ya nyumba na kuishi kila siku, hata katika maisha ya familia ambazo ziko karibu ili kugundua nguvu ya Injili ambayo ni kama Injini. Labda leo tumegundua katika familia ufunguo wa zamani,siyo tu tatizo la kutatuliwa, lakini ki ukweli inataka kuonesha mwanga mpya wa jamii ambayo inaweza kuwa harufu nzuri ya Injili katika familia. Kwa hiyo ratiba ya Mkutano wa IX wa dunia wa familia itaanza na ufunguzi tarehe 21 katika majimbo yote ya Ireland, tarehe 22-24 utakuwa ni mkutano, tarehe 25 ni tamasha la Familia na 26 Agosti, Ibada kuu ya misa ya kufunga Mkutano huo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.