Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maendeleo

Wasalesian wasaidia watoto barabarani mjini Addis Abeba

Mkurugenzi wa Kituo John Bosco cha Vijana Addis Abeba anawshukuru wadau na wafadhili wanaoendelea kuwasaidia ili vijana waweze kupata mwanga wa maisha yao ya baadaye. - REUTERS

21/08/2017 15:47

Shirika la Wasalesiani na Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuthibiti madawa ya kulevya na kuzuia ualifu (Unodc) wanashirikiana  pamoja kwa muda sasa  kwa ajili ya kuwasaidia vijana  barabara mjini Addis Abeba. Nia kubwa ni kuwapa mtazamo mpya wa maisha na kuwaondoa katika njia mbaya za unyonyaji, unyanyaswaji na ualifu wanaoufanya ili waweze kuishi . Ongezeko la watoto walioachwa peke yao na wengine kukimbia njaa ni janga kubwa linalo athiri jamii ya Ethiopia.Kwa njia hiyo Novemba 2015 Shirika la Mtakatifu John Bosco kwa kushirikiana na Ofisi ya umoja wa Mataifa ya kuthibiti madawa  ya kulevya na kuzuia ualifu , walianzisha pamoja kituo cha kupokea na kuwasaidiwa waathirika wa migogoro ya  ndani ya nchi hiyo kwa kufuta sheria.Tangu wakati huo vijana wengi wasichana na wavulana wanaishi katika kituo cha makaribisho cha Mpango wa watoto wa John Bosco chini ya  uangalizi wa watawa wa Shirika hilo.

Taarifa kutoka kwa muhusika wa utume wa Kimisionari wa wasalesian kutoka New Rochelle,Marekani, Padre Mark Hyde amesema,kwa upande wa mji wa Addis Abeba tu kuna watoto zaidi ya 100 elfu wanye kuwa na mahitaji ambao hawana msaada na wanaishi barabarani. Kutokana na Kituo cha watotoJohn Bosco  kuwa  kimoja katika mji huo kuweka nafasi ya mapokezi ni shida kubwa kukabiliana na kipeo hicho. Pamoja na hayo ushirikiano huo  unajitahidi kutoa chakula na vifaa vya elimu na  mahitaji binafsi ili kuweza kuwasaidia idadi kubwa iwezekenavyo ya watoto hao wadogo barabarani.
Hali kadhalika naye Mkurugenzi wa kituo hicho Andualem Tafesse, amesema kuna watoto ambao wameachwa peke yao au kuuzwa na wazazi wao ambao baadaye wanaishia magereza kutokanavitendo vya  ualifu na wizi. Vijana wengine wanafanya ualifu makusudi wakitegemea kwamba, kwenda magereza ndiyo njia ya kukidhi haja zao za mahiji msingi.  Lakini watoto hawa wanapo acha magereza hawana mahali pa kwenda, wanaishia tena barabarani. Hii ni hali mbaya inayodi kuendelea na kuzidisha umaskini, na mahangaiko ya hapa na pale , na sababu kubwa ya kujiingiza katika omba barabarani mkate wa kula kwa ajili ya siku. 

Katika kituo cha makaribisho, vijana hawa wanapata chakula, nguo za kuvaa , aidha  kuwawasindikiza katika mchakato wa kisaikolokia na kuwapatia kozi ya mafunzo ya kusoma na kuandika. Wakiwa tayari ndipo wanaweza kuwaelekeza katika mwelekeo wa mafunzo ya ufundi mbalimbali kama vile ufundi ujenzi, magari,  uselemala, kupika na kushona; kila mmoja kadiri ya uwezo alio nao. Kwa namna hiyo kituo hicho ni kwa ajili ya kuwasadia waweze kujitegemea wao wenyewe baada ya kutoka katika kituo hicho. Hiyo ndiyo lengo kuu la mafunzo ya kituo ambapo pia watawasaidia vijana hao kwa miezi mitano kiuchumi mara baada ya mafunzo wakati wakiendelea wenyewe kutafuta ajira na mahali pa kuishi kwa kijitegemea.

Hadi sasa matokeo ya vijana ambao wamepata kufaidika katika kituo hicho wanatoa shukrani kwa kujitolea kushirikiana na wahudumu wa kituo kwenda usiku kuwatafuta vijana wenzao wanaolala barabarani ili waweze kuja katika kituo hicho . Wanawatia moyo ili waweze ufika na kusaidiwa na kituo hicho.
Mkurugenzi wa Kituo anamaliza akisema, wale ambao wanaishi katika barabara wanayo shahuku ya kuweza kuishi katika jamii lakini wakati mwingine hawajuhi wafanye nini. Hata hivyo anawashukuru sana  wafadhili wengi na wadau wote wanao endelea kujikita katika kuwezesha mradi wa kituo hicho cha vijana na hatimaye waweze kuona njia mpya za maisha yao. 
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

21/08/2017 15:47