2017-08-21 15:16:00

Papa: Ombeni bila kuchoka kama ile sala ya mwanamke Mkananayo


Injili ya Jumapili Mt 15,21-28) inawakilisha mfano wa imani wakati Yesu  alipokutana na mwananamka mkanaani, huyo alikuwa mgeni  kwa upande wa wayahudi. Tukio hilo limetokea  wakati Yesu atembea kuelekea miji ya Tiro na Sidoni Kaskazini Magharibi mwa Galilaya. Hapo ndipo mwanamke huyo alisimama na kupaza sauti yake kwa ajili ya kuomba uponywaji wa mwanae, kama Injili inavyoelekeza kwamba alikuwa anasumbuliwa na pepo. Mara ya kwanza Bwana alifanana kama vile hakusikiliza kilio cha uchungu hadi kifikia kitendo cha mitume wake kumwomba kwa ajili yake. Lakini pamoja na majibu tofauti aliyo yatoa Yesu, mwanamke huyo hakukata tamaa ya kuendelea kuomba.

Huu ni utangulizi wa mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko Jumapili 20 Agosti, 2017 aliyoyatoa katika sala ya Malaika wa Bwana Mjini Vatican;Baba Mtakatifu Francisko amesema nguvu za ndani ya mama huyo  zinamwezeka kushinda kila aina ya vizingiti ambavyo vipo ndani ya upendo wa umama, na katika matumaini kwa Yesu ambaye anaweza kusikiliza na kujibu maombi yake.Baba Mtakatifu amesema hii inamfanya afikiri nguvu za akina mama. Katika nguvu zao wanao uwezo wa kupokea yaliyo makubwa; wapo wengi wanao tambulika.Kwa njia hiyo ni kusema kwamba ni upendo unao toa msukumo wa imani, na imani inageuka kuwa tunu ya upendo. Ni upendo mkuu unao mfanya apaze sauti yake kwa ajili mtoto wake, anapaza sauti akisema, “mwana wa Daudi nionee huruma”. Ni imani timilifu kwa Yesu inayo msaidia asikate tamaa hata mbele ya kukataliwa au kutojali mwanzoni; ndiyo maana mama huyo alikuja mbele yake akasujudu na kusema Bwana nisaidie.

Hatimaye kwa uvumilivu mkubwa wa mwanamke huyo, Yesu alibaki na mshangao mkubwa wa imani ya mama  mpagani. Kwa hiyo Yesu akamjibu, “mama imani yako ni kubwa basi fanyiwa kama unavyotaka “.Na Yule binti yake akapona wakati huohuo.
Unyenyekevu wa mwanamke huyo, Yesu ameounesha kuwa ni mfano wa imani isiyo tenguka kamwe. Uvumilivu wa kuomba msaada wa Yesu bila kikomo ni chachu kwetu sisi kutufanya tusikate tama, wala kuhangaika hasa wakati tunapokumbana na majaribu mengi ya maisha. Bwana hageukii upande mwingine mbele ya mahitaji yetu, hata wakati mwingine tunapofikiria kwamba hasikilizi maombi yetu; hiyo ni kutaka  kuimarisha imani yetu katika majaribu hayo. Wote tunapaswa kuendelea kupaza sauti kama huyo mwanamke, “Bwana nionee huruma , Bwana nionee huruma”. Sauti hiyo iwe ni kwa uvumilivu na ujasiri, huo  ndiyo ujasiri unao hitajika katika sala.

Ameendelea kueleza Injili hiyo Baba Mtakatifu Francisko akionesha ni kwa njia ipi tuweze kuimarisha imani akisema, tukio hilo la kiinjili linasaidia kutambua vema kuwa wote tanayo mahitaji ya kukua katika imani, na kuhimarisha matumaini kwake Yesu. Yeye anaweza kutusaidia kupata njia, hasa tunapopoteza mwelekeo huo wa njia katika safari ya maisha yetu. Katika njia hiyo inayooneka kuwa pana lakini iliyo jaa uchungu, hata tunaopoona ugumu wa kuwa waaminifu katika shughuli zetu. Ni muhimu kupalilia na kulisha imani yetu kila siku katika kusikiliza neno la Mungu kwa makini, kuadhimisha sakramenti mbalimbali na sala binafsi, tukipaza sauti kwake yeye tukisema, “Bwana nihurume”,  vilevile kwa njia ya kufanya upendo wa dhati kwa ajili ya wengine.
Amemalizia mahubiri yake Baba Mtakatifu Francisko akisema, ni kuomba Roho Mtakatifu ili aweze kusaidia kuwa na uvumulivu katika imani. Ni roho Mtakatifu anaye ongoza waamini wake ili waweze kuwa na  maisha yao kama mashihidi wa kweli wakristo wenye kuwa na nguvu ya kupokea na kufuata, ni roho wa Mungu anayetia moyo wa kushinda majaribu ya kutokumwamini Mungu pia  utofauti dhidi ya ndugu zetu. Naye Bikira Maria atuwezeshe daima kutambua mahitaji yetu kwa Bwana kwa njia ya Roho wa Mungu. Atusaidie tuwe na imani yenye nguvu, iliyo jaa upendo na upendo wenye uwezo wa kuomba kwa ujasiri kwa Mungu. 


Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko ametoa masikitiko yake kwa ajili ya mashambulizi ya kigaidi yaliyojitokeza katika siku hizi ambayo yamesababisha waathirika wengi, huko Burkina Faso, Hispania, na Finland. Amewataka kuwaombea warehemu wote, majeruhi  na familia zao. Ameomba kwa Bwana Mungu wa huruma na amani aweze kuokoa ulimwengu huu ulio jaa ukatili usio wa kibinadamu. Ameomba mahujaji pia walio kuwa katika viwanja vya Mtakatifu Petro kusimama kidogo kwa kimya na kuomba . Na baada ya ukimya huo amewasalimia mahujaji wote kutoka pande zote za dunia walio udhuria sala ya Malaika wa Bwana kwa pamoja.


Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.