Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Amani

Mitandao Katoliki ya kupinga nyanyaso yadai kuachiwa huru Rukuki Burundi

Hata hivyo Acat inasema kuwa wanaamini kwamba mashtaka yaliyo wasilishwa dhidi ya mwanaharakati huyo Germain Rukuki kutishia hali ya usalama wa Taifa ni kama kisingizio tu cha kutaka kupinga shughuli nyeti za kutetea uhuru na haki za binadamu zinazofanyika ndani ya mtandao Katoliki wa Acat

18/08/2017 13:57

Mitandao Katoliki wa kupinga nyanyaso  (Acat ) nchini Italia umeungana na tamko lilitolewa na Fiacat na Acat nchini Burundi kwa ajili ya kuachiwa  huru Germain Rukuki , mwasibu msatahafu wa Acat nchini Burundi aliyekamatwa kiholela na wahusika wa mambo ya ndani ya Serikali ya Burundi  tareh 13 Julai 2017. Kwa kipindi cha siku 14 za kuwekwa kizuizi , Rukuki hakuweza kupata nafasi ya kuongea na mwanasheria yoyote, na tarehe 26 Julai alihamishiwa katika gereza la Ngozi.

Tarehe 1 Agosti Rukuki alisikilizwa na Mwanasheria Mkuu Adolphe Manirakiza, ajulikanaye kwa shughuli zinasohusiana na ripoti za Kisiasa. Hata hivyo Acat  inasema  kuwa wanaamini kwamba mashtaka yaliyo wasilishwa dhidi ya mwanaharakati huyo Germain Rukuki  kutishia hali ya usalama wa Taifa ni kama kisingizio tu cha kutaka kupinga shughuli nyeti za kutetea uhuru na haki za binadamu zinazofanyika ndani ya mtandao Katoliki wa  Acat.

Hata hivyo Acat yenyewe ilikuwa tayari imeshakumbana na vizuizi vya  shughuli zake kutoka Mamlaka ya Burundi Novemba 2013 na baadaye kufutwa kabisa tarehe 28 Desemba 2016.Mbele ya mwanga wa matukio hayo, Acat ya Italia inaomba bila masharti kuachiwa  huru wa Germain  Rukuki , kwa kufanya rufaa kwa serikali ya Burundi na wadau wote wa kimataifa wenye kuwa na uwezo wa kuchukua hatua ya kuachiwa  uhuru huo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican 

 

 

18/08/2017 13:57