2017-08-18 13:41:00

17 Agosti nchi ya Indonesia yaadhimisha miaka 72 ya uhuru wake


Baada ya nchi ya India na Pakstani kuadhimisha siku ya Uhuru, mapema wiki hii tarehe 14,15 Agosti, hata nchi ya Indonesia tarehe 17 Agosti wameadhimisha miaka 72 ya Uhuru wake. Leo hii nchi ya Indonesia ni ya kidemokrasia yenye kuwa na idadi kubwa ya waislam. Kwa namna hiyo upo umakini kwa wale wote wadau wanao hamasisha mazungumzo kati ya wakristo na waislam. Kwa upande wa uchumi nchi ya Indonesia leo hii ina ushindani mkubwa  katika bara la Asia kutokana na kwamba nchi ya  kwanza ni Cina katika njia za kutafuta namna ya kuendeleza uchumi. Ikiwa imeundwa katika kisiwa kusini mwa Asia, Indonesia ni nchi ya nne ya kuwa na watu wengi duniani. Lakini pamoja na kuwa na maendeleo kwa miaka ya hivi karibuni, nchi hiyo bado inaendelea kuwa na tabia matabaka. Hiyo ni kwasababu mikoa iliyo mingi inakumbwa na utapia mlo, ukosefu wa jira na ukosefu wa usalama.

Kwa mfano inasemekana kuwa  milioni 7,7 ya watoto chini ya miaka mitano ambayo ni asilimia 36,8 wanateseka na njaa. Aidha ukosefu wa huduma za afya na maji ni  mambo yanayosababisha kuongezeka utapia mlo. Hali kadhalika ukosefu wa maji salama kutoka katika vyanzo vya maji ya kunywa na hakuna vifaa vya kuhakikisha usalama huo.Nchi hiyo pia mara kwa mara ina imekuwa na matatizo makubwa  ya majanga ya kiasili kama vile tetemeko la ardhi, mafuriko, kimbunga, ukame na maporomoko ya ardhi

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

 








All the contents on this site are copyrighted ©.