2017-08-17 10:00:00

Watu wa Iraq wanayo matumaini pamoja na giza la siku za usoni


Jumuiya ya Kikristo  nchini Iraq imefanya sikukuu ya Mama Maria kupalizwa mbinguni  tarehe 15 Agosti 2017 kama vile nchi jirani ya Siria, ambayo ameeleza Balozi wa Papa huko Damasko Kardinali Mario Zenari. Ni tukio ambalo Kanisa katika nchi hiyo waamini wake wamekusanyika kusali , japokuwa na hofu zinazojitokeza katika kila adhimisho la wakristo kutokana na ghasia mahalia zitokanazo na Serikali ya Kiislamu. Katika miaka miwili ya mwisho maeneo mengi ya nchi yamekumbwa na mashambuliz ya kigaidi. Katika makambi ya kivita matukio ya kila siku yanazidi,  kwa mfano mapema wiki hii  mwanajeshi wa Marekani ameuwawa na wengine watano kujeruhiwa huko Kaskazini kwa nchi. Taarifa kutoka kwa wanajeshi wa Iraq wanasema hiyo ilikuwa ni ajali iliyosababishwa na kulipuka kwa bomu wakati wakifanya mazoezi ya kijeshi. Baada ya kero za Mosul dhidi ya serikali ya Kiislam , wanajeshi hao wamehamia katika eneo la Tal Afar kaskazini mwa Iraq. Wakati huo huo  mamia ya maelfu ya raia wameanza kurudi katika vijiji jirani baada ya maeneo hayo kukombolewa. Ni operesheni uliyofanywa pamoja na mashirika ya  kibinadamu kuwawezesha mapambano ya wanajeshi wa Serikali wanaotafuta kuwashinda hayo majeshi ya kijihadi.

Hata Askofu Mkuu wa Baghdad Jean Benjamini Sleiman anasema jinsi wanavyokabiliana na wahamiaji, japokuwa ni wachache kama ilivyokuwa inatarajiwa familia zilizorudi katika vijiji vilivyokombolewa. Na katika kuadhimisha  Sikukuu ya Kupalizwa mbinguni mama Maria, Askofu Mkuu amesema, watu wengi wamejisikia kuwa na matumaini katika makanisa yote yanayo adhimisha sikukuu hiyo ijulikanayo kulala usingizi Mama Maria katika makanisa yote ya Kiorthodox. Sikukuu hiyo nchini Iraq imandaliwa na waorthodox ambao tangu mwanzo wa mwezi walianza na mfungo uitwao mfungo wa Bikira mpalizwa, kwa maana hiyo ni maandalizi ya kina ya kiroho.
Aidha pamoja na maandalizi ya sherehe hizi, hofu haikukosekaana , ambayo ameita kuwa ni ugonjwa wa hofu sugu kwa sasa. Ni hofu lakini haikuwa kama ile ya kuzaliwa kwa Bwana na Pasaka .Aidha anamesema, nchini Iraq kwa siku kama hiyo ni siku ya kazi ambapo wakristo wanalazimika kutafuta muda wao wa kwenda Kanisani kwa maana ya  alfajiri au jioni baada ya kazini. Lakini  ni katika nchi zote za Mashariki, ispokuwa nchi moja ya Lebanon ambayo siku hiyo ni ya Kitaifa.

Askofu Mkuu anaelezea juu ya hali halisi ya maisha nchini Iraq ambayo siyo rahisi na hasa kwa kuzingatia maisha ya baadaye, kwamba  bado ni giza . Hiyo ni kutokana na kwamba maisha yao bado ni ya kuendelea kuishi kwa kuhama hama kwa watu wengi na ambao wanazidi kuondoka kwenda mahali pengine, hakuna mwanga wa maisha endelevu kwa sasa. Aidha amesema, kuna baadhi ya sehemu zilizokombolewa na familia zinarudi katika maeneo yao, lakini siyo watu wengi ambao walitegemewa. Yote hiyo ni kutokana na matatizo ya kisiasa katika maeneo ambayo hayana matumaini na ukosefu wa watu kuaminiana kati yao. Na isitoshe hali ya upungufu wa watu imezidi kuonekana hata  makanisani tangu mwezi wa sita hadi leo. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.