Kuridhika na kufurahi ni hisia ambayo Kanisa Katoliki la Ufilippini limeonesha wakati wa kupokea taarifa ya kupitishwa kwa mswada wa bunge ya nchi hiyo wenye lengo la koboresha hali ya maisha ya maskini na wanyonge katika nchi. Kupitishwa kwa sheria hiyo unaweza kuifanya Serikali kutoa kipaumbele katika mipango inayojikita katika maskini hasa sekta ya chakula, nyumba na maisha bora, elimu na afya.
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Manila Broderick Pabillo,kuhusiana na rasimu ya Sheria
hiyo ameilezea kwamba ni kama moyo mkuu wa maskini, ni kipimo muhimu ambacho kinaonesha
kutokusahau maskini,hivyo ni matumaini yake kwamba pendelezo hilo linaweza kuwa sheria
timilifu kwa mambo yote .
Kwa upande wa Padre Edwin Gariguez ambaye ni mwanachama wa Sekretarieti ya Taifa kwa
ajili ya shughuliza za Baraza la maaskofu mahalia, amesema, serikali inapaswa kutenda
kwa haraka iwezekanavyo ili kupunguza umaskini nchini humo.
Hiyo yote ni kutokana na taarifa za kusikitisha kuwa, janga la umaskini katika nchi ya Ufilippini inakithiri kiasi kikubwa zaidi cha kuwafanya watu wengi wa Ufilippini kulazimika kuuza hata viungo vyao katika nchi tajiri za magharibi wanaotafuta kwa udi na ufumba matibabu. Kwa mujibu wa takwimu za serikali huko Manila, inasadikika kuwa, ni watu karibia elfu tatu wamehusika katika miaka ya hivi karibuni kwenye biashara haramu ya kuuza viungo kinyume cha sheria.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |