2017-08-16 09:18:00

Vijana Afrika ya Kusini waanza kujinoa kwa Siku ya Vijana Duniani!


Katika mbio za maandalizi ya kuadhimisha siku ya Vijana duniani nchini Panama mwaka 2019, hata Baraza la Maskofu wa Afrika ya Kusini wamependekeza kufanya maandalizi madogo ya siku hiyo ya vijana katika nchi yao, ikiwa na lengo la kuwaandaa kikamilifu vijana, itakayo fanyika kuanzia tarehe 3 hadi 10 Desemba 2017 huko Durban. Maandalizi hayo ya kufanya Siku ya vijana ndogo katika nchi ya Afrika ya kusini ina lengo la kuweza kuwapata na  kuwapeleka vijana wengi washiriki Siku ya Vijana duniani.Kwa kufanya hivyo ni kuwasaidia vijana wazoee na wafanye uzoefu wa aina yake ambao utaweza kuwashirikisha vijana kutoka Afrika ya Kusinini, Botswana, Swaziland, Lesotho, Namibia,Malawi na Zimbabwe. Kwa njia hiyo Maaskofu wanatoa wito kwa  kwa maparokia yote ya nchi hizo ili waweze kushirika kwa dhati katika maandalizi hayo kwa kuwasaidia vijana washirikishishane ushuhuda na historia na wenzao wa rika lao.

Kwa  mujibu wa jimbo la Pretoria, vijana ni viongozi wa Kanisa la kesho na hivyo hawana budi kutambua nafasi yao zaidi waliyo nayo. Tukio la huko Durban lenye kuwa na lengo la kuwafanya vijana waweze kuudhuria kwa wingi huko Panama katika Siku ya Vijana Duniani inayotarajiwa kuanzia tarehe 22 hadi 27 Januari 2019 kwenye nchi hiyo ambayo katikati ya Amerika, itawatia moyo na ujasiri wa kuweza kushiriki kikamilifu. Pamoja na taarifa hiyo nzuri ya mpango wa kufanyika hiyo Siku ya Vijana nchini Afrika ya Kusini bado kuna isemayo kuwa inabidi kutambua hali halisi ya vijana wa Afrika ya kusini siyo kati ya hali zilizo bora: hiyo ni kwasababu ya mamilioni ya vijana kukosa kazi.

Hayo ni maelezo yaliyo kuwa katika ujumbe wa Askofu wa Jimbo la Kimberly Abel Gabuza ambaye ni Rais wa Tume ya Haki na Amani ya  Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kusini. Katika ujumbe huo alikuwa akitoa wito kwa serikali kwasababu ya kipeo cha ukosefu wa ajira kwa vijana katika nchi yao. Alisema hali hiyo imefikia ngazi ya hatari kwa vijana wasio na kazi ambao wako hatari ya kumezwa na kuathirika na madaya ya kulevya, biashara haramu ya binadamu, na kujiingiza katika makundi ya kialifu na zaidi kushawishiwa kwa upande wa kisiasa wasio kuwa na haibu ya kuwaadaa wajiingize kwenye migomo ya kuleta vurugu na ghasia.

Sr Angela Rwezaula.
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.