2017-08-14 09:51:00

Yesu anafundisha kushirikishana hasa na wahitaji wote duniani


Tuwe na ujasiri wa kutoka kwenda kukutana na wangine , hata kwa zana dhaifu ambazo hazinunuliwi. Hiyo ni kutumia muda wetu ambapo  nyakati za sasa ni  jambo muhimu japokuwa tayari katika ulimwengu huu unaotoa msukumo zaidi wa kupoteza wakati. Ni maandishi yaliyo andikwa na Frateli Alois  Mkuu wa Jumuiya ya kiekumene ya Taize kwenye Gazeti la Osservatore Romano tarehe 12 Agosto 2017.Ameyaandika hayo akiwa katika maandalizi ya kukutana na vijana kutoka pande zote za dunia kwenye  Jumuiya yao ya sala nchini Ufaransa. Kati ya vijana walio unganika  nchini Ufaransa  katika  sala wapo karibia vijana 120 kutoka katika Bara la Asia, Afrika, Amerika ya Kusini na nchi jirani za Mashariki.

Mkuu wa Jumuiya ya Kiekumene ya Taize ameandika ; kipindi  cha kiangazi kimeonesha mwamko wa imani ya vijana wakristo wengi wa kiarabu kutoka nchi ya Misri, Palestina, Jordania na Lebanon waliofika katika jumuiya yao: Na mwisho wa mwezi wa Septemba mwaka huu, baadhi ya frateli wa Jumuiya ya Taize watakwenda  na mamia ya vijana wa Ulaya na Mashariki ili kufanya uzoefu  wa kushirikishana kwa  sala na vijana wengine nchini  Misri.Wote kwa pamoja , anasem Frateli Alois  wanaweza kufanikiwa kuishi  kwa sala na maombi na kushikirikishana katika mlima, kwa  mfano wa Yesu ambaye kafufuka.

“Tunapoweka matumaini na imani yetu kwake yeye anatufanya tuwe  mashuhuda wa upendo wake. Ni yeye anayetufundisha namna ya kushirikishana mbele ya mateso ya binadamu, unyenyekevu wa umasiki na katika majaribu mengi kwa wale wasio kuwa na nyumba na wahamiaji”. Mkuu wa Jumuiya ya Kiekumene ya  Taize anamalizia na fikra za Baba Mtakatifu Francisko ya kwamba anao utambuzi wake juu ya kutia moyo. Anasema, siyo tu kwa wakristo peke yake, bali ni kwa watu wote ambao wanatiwa moyo mkuu  na Baba Mtakatifu Francisko: “Yeye anafanya matumaini ya amani ya binadamu yachanue. Kwa njia hiyo anawaalika vijana kusali kila siku kwa ajili ya amani.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.