2017-08-14 13:45:00

Mashirika yasiyo ya Kiserikali kusitisha operesheni bahari ya Mediterranea


Baada ya Madaktari wasio na Mipaka na Shirika lisilo la Kiserikali ya Ujerman (Sea Eye), hata Shirika lisilo la Kiserikali la Saidia Watoto (Save the Children) limesimishwa uendeshaji wa kokoa wahamiaji  katika Bahari ya Mediterranea.  Mashirika haya ya Kibinadamu yako katika kutafakari zaidi mara baada ya tamko la kutoka Mamlaka ya Serikali nchini Libia,ambapo wametaka kudhibiti na kuzuia Meli za mashirika yasiyo katika maji ya kimataifa. Ni mahali ambapo hata meli nyingine zimesimama katika Kisiwa cha Malta wakisubiri kujua hali ya usalama kabla ya kuendelae na operasheni zao. 
Shirika la Saidia Watoto (Save the Children) wanalalamika kutokana na kulazimishwa kusitisha operesheni hiyo ya  kuokoa watu Bahari ya Mediterranea. Ujumbe unasema, ni hali ya kusikitisha kwa sababu ya hatari ya usalama wa wafanyakazi na kwa ajili ya uwezo wa hali ya Meli ya Vos Hestia kutekeleza uokoaji wake. Katika hali hii mpya, Shirika la Kusaidia Watoto (Save the Children) inasema boti za wahamiaji watalazimika kurudi Libya wakati huohuo watoto wengi na vijana watakufa kabla ya kuacha eneo jipya la Sar ya Libia.

Mkurugenzi wa Uendeshaji, Rob MacGillivray anasema, Shirika la Kusaidia Watoto liko tayari kuanza tena shughuli zake kuokoa eneo hilo, lakini wanawajibu wa kuhakikisha usalama wa timu yao na ufanisi wa utendaji. Kabla ya kuweze kuendelea na operehseni hiyo ni lazima kuwa na uhakika hasa juu ya usalama wa wafanyakazi wao amesema. Save the Children pia wanao wasiwasi  mkubwa kuhusu kupungua kwa uwezo wa nguvu za uokoaji baharini kutokana na kusimamishwa kwa shughuli hata za mashirika mengine katika Mediterranea. Anasema kuwa wao wanelewa na  kuheshimu mashirika yote yasiyo ya kiserikali katika hali hiyo ya kuchukua uamuzi mgumu ambao wanajikuta katika hali hiyo.
Amemalizia akisema, kusitishwa kwa uperesheni za meli katika kuokoa watu inahatarisha maisha ya binadamu na kupunguza uwezo wa kuwasadia watu kwa njia hiyo ni muhimu  kuanza kwa upya  operesheni hiyo mapema iwezekanavyo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.