2017-08-14 09:27:00

Korea:Maaskofu wamewataka viongozi wa nchi mazungumzo ya amani


"Baada ya uzinduzi wa kombora Hwasong-14, Peninsula ya Korea iko katika hali ya wasiwasi na uwezekano wa hatari kubwa. Majaribio ya silaha za nyuklia huko Korea ya Kaskazini zinaonekana wazi ukiukwaji wa azimio lilokuwa limetolewa  na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa njia hiyo ni hatua inayojaribu kuhatarisha amani ya Asia ya Kaskazini na kuwataka silaha za nyuklia katika nchi jirani . Hii ni taarifa iliyo andikwa na Baraza la Maaskofu nchini Corea, iliyopelewa na Shirika la GHbari la Sir . Wameandika Ujumbe huu kwa umma kwa ajili ya tukio la Maadhimisho ya mwaka wa 72 wa uhuru wa Korea utakaofanyika tarehe 15 Agosti 2017.

Ujumbe wa Baraza la Maaskofu nchini Korea unasema, Kanisa la Korea linakemea matendo yasiyostahili ya Korea ya Kaskazini ambayo ni kinyume kabisa na maazimio, ambapo matendo hayo yanazidi  kuongezeka katika Peninsula ya Korea na kuifanya kurudi nyuma katika kuendeleza  amani. Ujumbe unahakiki kwamba  kutumia silaha za nyuklia siyo ufumbuzi wa busara. Kwa njia hiyo wanahimiza viongozi wa kisiasa wa Korea ya Kaskazini kuanzisha mazungumzo ya amani na kufanya kila iwezekanavyo hata ikiwezakana kuanzisha mfano taasisi  ili kuhakikisha amani ya Peninsula  kwa njia ya ushirikiano na nchi jirani.

Aidha Ujumbe huo wa maaskofu wanasema, “kuzungumza  juu ya vita bila kuzingatia hatari ni hatua za vurugu dhidi ya ubinadamu. Kufanya matendo ya kurupuka  bila breki, zinazoonyesha  hali ukatili na uwenda wazimu, hatatakubali watu wengi wafe vifo hivyo ambavyo pia vitaleta uhalibifu kwa pande zote mbili maana ni kurudi nyuma katika historia ya binadamu na kuleta majeraha makubwa ya  binadamu wote”. Kwa njia hiyo wanahimiza nchi zote jirani kutokuchukua uamuzi usio kuwa na busara ambao unaweza kutishia upendo na maendeleo ya kimaadili na kiroho kwa binadamu. Na kwamba wanayo matumaini ya viongozi wakaweza kutafuta suluhisho kwa njia ya kidiplomasia na kisiasa.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.