2017-08-14 14:08:00

12 Agosti,Siku ya Vijana Kimataifa kwa kauli mbiu Vijana wanajenga amani!


Tarehe 12 Agosti 2017 Tume ya  nchi za Ulaya huko Bruxelles imeungana  kwa pamoja kuadhimisha Siku ya Kamataifa ya Vijana, ambayo ilikuwa na kauli mbiu “ Vijana wanajenga amani”. Tume ya Umoja wa nchi za Ulaya imeonesha kwa namna ya pekee mchango ambao vijana wanaweza kujikita katika kuendeleza mbele  kwa ajili ya kuzuia na kubadili maisha katika ushirikishwaji wa haki za kijamii na amani endelevu.Kamishna wa Umoja wa nchi za Ulaya wa Elimu,Utamaduni ,vijana na michezo Tibor Navracsics katika hotuba yake amesema, inawezakana  kufikia amani endelevu na kujenga jamii yenye mshikamano na ujasiri kama kila mtu  anafanya kazi kwa pamoja. Vijana wameonyesha kufanya kazi katika hali ya mshikamano, na kusaidia kujenga jamii zao. Ni lazima kuweka matunda ya nguvu zao hizo. Hata Kamishna wa Ushirikiano wa Kimataifa Bwana Neven Mimica aliongeza kusema, vijana ni kiini cha maendeleo, kwa njia hiyo, shukrani kwa nchi za Umoja wa Ulaya  ambapo kwa miaka 10 iliyopita karibia milioni 14 za vijana wavulana kwa wasichana wamepata elimu ya msingi na wataendelea kuwasaidia vijana waweze kuwa mabingwa wa amani.

Siku ya Kimataifa ya Vijana ni tukio muhimu la kukumbuka njia mbalimbali ambapo Tume ya Umoja wa nchi za  Ulaya inajikita katika matendo ya dhati kwa ajili ya kuwasaidia vijana . Kwa mfano, kiungo cha Ulaya kwa ajili ya mshikamano  ambacho kimeunda nafasi ya pekee kwa ajili ya vijana kati ya miaka 18 na 30 ya kushiriki katika aana mbalimbali za shughuli za mshikamano kwa nchi zote za Ulaya. Tangu uzinduzi  wake mwezi Desemba mwaka Jana ni zaidi ya vijana 34 elfu wamejisajiri  na mamia ya vijana tayari wamekwisha anza miradi yao. Aidha taarifa imesema kuwa mwaka huu pia wamesheherekea miaka 30 tangu uanzishwe mpango wa Erasmus. Huu ni mpango mmojawapo wa ki historia wenye kuwa na mafaniko. Hadi sasa mpango  wa Erasmus na waliotangulia wamefikia milioni 9 za wanafunzi wa  Ulaya nzima. Hawa wote wameweza kupata fursa ya nafasi ya kujifunza, kufanya kazi ya kujitolea , kupata uzoefu wa kitaalamu nje ya nchi, kujenga kizazi  wazi katika kutambua changamoto za Ulaya  za ulimwengu  mzima kwa ujumla.

Wakati Tume ya Ulaya inaadhimisha siku ya Kimataifa ya Vijana hata katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, siku hiyo hata vijana kutoka pembe tofauti za dunia waliowakilisha kundi  la vijana wanaokadiriwa kuwa bilioni 1.8 kote duniani, walijadili umuhimu wa kukabiliana na umaskini, kujenga uchumi  unaojali mazingira. Halikadhalika wazungumzaji wamehamasisha umuhimu wa ujumuishwaji wa vijana katika maendeleo hususani utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. Hiyo ni kwasababu kuna haja ya Umoja wa Mataifa kuwashirikisha vijana na kupata mtazamo wao wa jinsi dunia inavyopaswa kuwa ifikapo mwaka 2030, ili hatimaye ni vijana hao  watakaongoza utekelezaji wa ajenda hiyo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.