2017-08-12 15:02:00

Wito na huduma ya Ushemasi wa kudumu nchini Italia kuongezeka!


Jimbo la Vincenza nchini Italia  linajianda kupokea Mkutano wa Kitaifa wa Mashemasi, utakao kuwa ni  Mkutano wa XXVII mwaka 2019 kama inavyonesha katika Barua ya kukubali ya Askofu wa Vincenza Beniamino Pizzol. Aliyetangaza habari hiyo ni Ris wa Kamati ya Mashemasi nchini Italia Enzo Petrolino wakati wa Mkutano wa mafunzo ya kina uliofanyika katika Kisiwa cha Cicilia kuanzia tarehe 2 hadi 5 Agosti kwenye Jimbo la Cefalu. 
Ni mtandao wa mashemasi, wa huduma , ya uinjilishaji na wa ubinadamu kwa mantiki ya dini jamii ya sasa. Ni mtandaoaambao unaotengeneza mtandao katika mitandao ya kijaami mahali ambapo pamekuwa umewawezesha kuwa na ufahamu na kuwasiliana pia wakiwa na lengo la kulinda huduma ya utume wa ushemasi. Kiini zaidi ni ile nafasi ya kuunda mtandao kwa ajli ya kutazama sura ya ushemasi, utume mpya wa kiroho  kwa kutazama zaidi jamii ambayo ya sasa mahali ambapo kuna mgawanyiko kutokana kipeo cha maadili.

Kabla ya Mkutano huo katika Jimbo la Cefalu huko Kisiwani Sicilia, Rais wa Mashemasi alikuwa amemwandikia Baba Mtakatifu Fancisko, akionesha ratiba kamili ya mkutano huo ambayo imehusu wajibu wa ushemasi  hasa ule wa kutoka kwenda njiani na ule utokanao na tunda la mkutano kuhusu kukaribisha; hali kadhalika kuhusu  kukusanya mtaji kwa ajili ya kununua Biblia katika lugha ya kingereza, na kifaransa, ili kuweza kuwagawia  wakristo wahamiaji ambao sasa ni sehemu ya Kanisa waliopokelewahuko Lampedusa na wengine waliongia nchini Italia. Aidha kutazama tukio la kuadhimisha Siku ya Wahamiaji tarehe 19 Novemba, ambayo Baba Mtakafifu Francisko ameiweka kwa ajili ya masikini. Hiyo ndiyo mojawapo ya utume wa shemasi kuacha kila kitu kwa ajili ya maskini ili waweze  kupewa kipamumbele katika kila liturujia ya ekaristi takatifu. Hiyo ndiyo ilikuwa wajibu mkubwa wa mkutano huo. Ni njia ambayo ni wazi kwa shughuli za utume wa safari ya imani ambayo mashemasi karibia 4,400 nchini Italia ambao kwa pamoja wanahudumia familia zao.

Mafunzo ya kudumu, kiroho, kichungaji na kiteolojia, imekuwa ni kiini cha mada za haraka cha kuzingatia ambapo  wahusika kwa kutoa  mafunzo hayo kwa mashemasia katika siiku hizi mbili  walikazania juu ya changamoto ya Kanisa inayokumbana nayo katika nyakati hizi, hasa kwa kwa kuzingatia kipengele cha tatu cha Furaha ya Injili ya Baba Mtakatifu Francisko. Tabia ya mkutano huo kwa kila baada ya miaka mitatu inatoa fursa ya kujikita ndani kabisa katika hali halisi ya Kanisa na Mashemasi nchini Italia, ambayo ni safari inayozidi kukomaa katika imani. Halikadhalika inatoa fursa ya kukomaa kiroho kama itajwavyo kwenye  waraka wa Baba Mtakatifu Francisko wa  Injili ya Furaha .Tendo la kuwasaidia wasikini,ndiyo jambo muhimu katika maisha ya utume na kuwa mstari wa mbele; Hayo pia amesisitiza Kardinali Montenegro Rais wa Caritas nchini Italia na Askofu Mkuu wa Agrigento. Wahamiaji , masikini, wagonjwa ndiyo wajibu wa mashemasi katika kujibidisha kwenye changamoto ya kutengeneza nyumba kwa ajili ya  kuonesha upendo. Kardinali Montenegro anasema,altare siyo lengo la  mwisho wa Mashemasi bali lengo ni ulimwengu kwasababu,uinjilishaji siyo kutangaza neno tu  bali maneno yaendane na vitendo. 

Shemasi analazimika kuchafua mikono yake, hiyo ni kutokana na kwamba  shemasi wa leo hii ndiyo wa jana ambaye anatazama mbali na kujenga matumaini ya Ufalme wa Mungu. Shemasi katika kukaribisha  anaonesha undugu, urafiki kwa njia ya kusikiliza kwa masikio, akili, moyo na macho. Shemasi analazimika kuchoka kwa upendo. Pamoja na changamoto anazokumbana nazo katika kutumika Kanisa, bado anatunza hata familia yake kama vile bibi  arusi ambaye ni kiini cha upendo na muungano wa Kanisa . Askofu Mkuu Montenegero aliwaeleza wake wa mashemasi walioongozana na waume zao katika Mkutano huo wa Ishirini na sita wa Kitaifa nchini Italia.Aidha wakati wa Mkutano huo,wapo baadhi ya wanawake waliotoa ushuhuda wa maisha yao; wao ni kiini cha kutambua na kusaidia miito katika nyanja muhimu za kijamii, aliongeza kusema Askofu Mkuu.
Kwa namna hiyo wote wamepeweza mwaliko hukoVincenza mwaka 2019 ili kuweza kuendelea kukabiliana na  changamoto mpya katika mwelekeo wa kizamani lakini  daima utaendelea kuwa mpya katika kutoa huduma ambayo ni sehemu kuu na uwajibu wa ushemasi. 

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.