Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Australia: Wahamiaji wanastahili heshima na maisha yao kulindwa

Serikali ya Australia inapaswa kulinda hadhi na heshima kwa wahamiaji na kuhakikisha usalama wao huko Manus - AFP

11/08/2017 16:15

“Wahamiaji na wakimbizi wanastahiili kupewa hadhi yao”. Ndiyo taarifa iliyoandikwa na Askofu Vincent Long Van Nguyen mwanachama wa Baraza la Maaskofu wa Australia na mjumbe katika Sekta ya wahamiaji na Wakimbizi. Kauli  ya maaskofu imewadia baada ya siku za hivi karibuni mkimbizi katoka kambi ya wakimbizi wa Manus huko Papua Guinea Mpya kukutwa amekufa na  Mwauame mwenye umri wa miaka 31 akiwa na asili ya Iran ambapo mwili wake uliokutwa katika msitu karibu na kambi hiyo.

Ujumbe unasema,waliofika  nchini Australia katika kutafuta usalama na maisha bora wanasahili zaidi wakati watu wanaotafuta hifadhi ndiyo wenye kuathirika katika jamii yetu ya kimataifa. Kwa  njia  hiyo ni muhimu kutoa kipaumbele na  kuwashughulikia ili wapate hadhi yao na zaidi lazima wawe na huru wa kuchagua mahali wanapotaka kwenda katika nchi zenye usalama ambapo hakuna mateso.Katika barua hiyo wanatoa wito kwa serikali ya Australia kutoa huduma na  msaada kwa wale wakimbizi wanaoishi katika kisiwa cha Manus wakisubiri ufumbuzi hadi sasa.Hata hivyo wanadai pia serikali ipitishe  mpango wa ulinzi kwa ajili ya wahamiaji ambao wanao tafuta ukombozi kwa kupitia njia ya bahari. Barua inasema ni muhuimu kuzuia kupoteza maisha ya watu baharini lakini pia umuhimu wa kuwa makini kwa watu ambao wanaishi katika kambi hizo, ambapo serikali ya Austaralia inapaswa kuwajibika kutoa makazi mengine mapya kwa haraka.

Ni muda mrefu sasa ambapo kumekuwa na mjadala kimataifa unao husu ukiukwaji wa haki za wahamiaji katika kambi la wakimbizi huko Manus ambapo wanasubiri kambi hiyo ifungwe.Kwa namna hiyo Barua ya Askofu Nguyen inatoa ombi kwa serikali ya Austraia kuheshimu wajibu wa Kimataifa, na kufanya kazi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuhakikisha usalama wa wale wanao tafuta hifadhi.
Ikumbukwe kuwa Canberra ilihukumiwa tayari kulipa Euro milioni 47 katika dola za Australia kama fidia  kwa ajili ya wanao tafuta ifadhi kati ya mwaka 2012 na 2014 huko Manus ambao walilalamikia utaratibu mbaya.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

11/08/2017 16:15