2017-08-11 15:11:00

Askofu Mkuu Fisichella ataka umoja na mabadiliko nchini Ufilippini


Ni ushauri wa kuondoka katika  nafasi uliyopo na kuelekea katika utume ambayo Askofu Mkuu Rino Fisichella amewashauri makatekista wote nchini Ufilippini kwenye tukio la kuwakilisha rasmi katiba ya chama kipya  kitaifa  (Nac-Phil)  kilichoanzishwa, kichounganisha wahusika wote katika shughuli za katekesi  Barani Asia.Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha unjilishaji mpya amekuwa huko siku za hivi karibuni Manila kwa mwaliko wa Askofu Robert C.Mallari Rais wa Kamati ya Katekesi na Elimu Katoliki katika Baraza la Maaskofu Ufilippini.

Askofu Mkuu Fisichella amesema, mara kwa mara huduma inayotolewa inawapelekea kujitambua nafsi zao walizo nazo ndani ya jamii, na hivyo anawaonya  makatekistakuwa  hawako nje ya kishawishi cha kutumia nafasi waliyo nayo kama vile ni kazi ya kudai chochote. Kinyume  anapaswa atambue kuwa huo ni utume wa kutumiza; kwasababu kuna utofauti wa wajibu wa kazi ambayo inahitajika kuhesabu masaa utume unahitaji kujitoa maisha yako yote. Kwa njia hiyo Mungu anapoingia katika maisha ya mtu hakuna uchaguzi mbele yake anachoomba ni ule utashi wa Imani na jibu la dhati lenye msimamo. Chama kipya cha makatekista huko nchini Ufilippini kinazidi kutanda mizizi hasa katika mafundisho  na shukrani kwa ushirikiano wa baadhi Taasisi za Kipapa  zinazoandaa mafundisho kipindi cha masomo ya mwaka wa shule kama  vile  Chuo Kikuu Maalumu cha De La Salle.Na ndiyo maana wakati wa hotuba yake Askofu Mkuu ametoa pongezi kwao,pia washiriki wote kutoka majimbo,vyama mbalimbali ,taasisi za kidini kwenye Mkutano huo wa kuawasilisha katiba mpya na mkutano ulikuwa na mada ya “makatekista , wajenzi wa umoja, na wakala wa mabadiliko”.

Aidha anasema "Wakati mwingine tunaamini kwamba katikesi ni moja ya matendo na mbinu za kutekelezwa, wakati huo huo kusoma na  mafunzo ni vinapaswa kutamia nyanja ya kiakili tu”. Kwa njia hiyo askofu anaonya;  kufikiri kwamba elimu ni kubaki umekaa mbele ya meza na kitabu mikononi kilochufunguliwa kwa kujiandaa na mitiahani au somo; manna yake ni kusema hujatambua nini thamani ya elimu”.Askofu Mkuu Fisichella anafafanua maana ya elimu akisema;hawali ya yote ni kurudia kushika mikononi mwako Neno la Mungu na kulifanya liwe kirutubisho cha kuishi. Ni  Neno hai ambali linatangazwa, ninaeleweka a daima na zaidi lenye kuwa na msingi halisi wa kuweza kuridhisha vizazi hadi vizazi hadi kufikia uhalisia wa dhati kwa kila nyakati.

Na zaidi ni kama waraka wa “Neno la Mungu” (Verbum Domini) usemavyo:   mafunzo yamewezesha jumuiya nyingi kuwapa maisha katika shule za Injili, tafakari, mazoezi ya imani na uzoefu mbalimbali wenye utajiri wa kihistoria za sasa  ambazao zimeunda katekismu.
Aidha baada ya kuwakumbusha kuwa mkutano wa katekesta wa Ufilipiini umekwenda  sambamba na Kanisa kuadhimia miaka 25 ya Katiba ya Kitume (Fedei Depositum) kwa ajili ya kutangaza katekisimu ya Kanisa Katoliki, Askofu Mkuu Fisichella amesema,watambue kwamba kadiri miaka unavyozidi kwenda mbele ndivyo kwenye matukio ya Mtaguso wa Pili wa Vatican unavyozidi  kuongezeka dharura ya kuendeleza ahai wa mafundisho ambayo Katekisimu inabaki kuwa tunda la Mtaguso. Hiyo pia ni kutokana na yeye mwenye kuwa Rais wa Baraza la kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji mpya, wenye kuwa na majukumu ya kila wakati kuhamasisha kufikiahata tafsiri za lugha zaidi ya 60. 

Askofu Mkuu Fisichella amelezea  suala la tabia za nyakati  zetu hasa  zile na uelekeo wa kuhalalisha ukweli wa kuwa mkristo bila kujali elimu na maadili ya Katekismu.Kwa njia hiyo yeye anasema hili ni tendo la hatari  zaidi ambalo mtu uamini kuwa na haki kwasababu anao utambuzi wa utume ambao anajitolea idhini yake. Kwa namna hiyo Askofu Mkuu anatoa umuhimu wa uinjiilishaji mpya ambao unaweza kusaidia kuondokana na matatizo yaliyopo katika Makanisa mbalimbali yakiwepo hata  katika Kanisa la Ufilippini, ambapo mara kwa mara wanapata vikwazo katika kufanya  katekesi ya maandalizi ya Sakaramenti. Kwa njia hiyo kuna haja ya mafundisho ya kudumu inayowalenga waamini wote , kuheshimu hatua mbalimbali na mbinuambayo inaeleweka na kufafanua zaidi watambue matendo ya kikristo kwa mtazamo wa maisha ya dhati na kile wanachokiamini.

Aidha Askofu Mkuu nasema, siyo kwa habati mbaya kusikia kwamba leo hii bado kuna maombi kutoka kwa wakatekumeni ambao wanafanya uchaguzi wa imani na kiakili ili kuweza kudumu na kutoa ushuhuda wa maisha ya kikristo. Hatimaye Askofu Mkuu Fisichella alisisititiza kuwa katekesi iwe wazi, na bora kwa maana ya uzoefu wa kuishi kijumuiya,mahali ambapo waumini wapate kushirikishana imani yao na kusaidiana wao kwa wao kwa kutoa ushuhuda mahali ambapo wanaitwa kila siku katika familia na kazini.Kutokana na umoja na ushirikiano, amewaonya makatekista ya kwamba hakuna katekista yoyote afanye huduma hiyo kwa njia ya binafsi bali daima ni ndani ya Jumuiya na kwa jina la Kanisa.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.