Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Elimu

Scholas Occurrentes kufika hata Afrika katika nchi ya Msumbiji

Scholas Occurrentes kufika hata Afrika katika nchi ya Msumbiji ambapo vijana 180 wa shule wamefanya uzoefu wa wiki moja hivi karibuni - RV

10/08/2017 16:08

Hivi karibuni umemalizika uzoefu wa Scholas Occurrentes  huko Missao Mangunze nchini Musumbiji. Kwa wiki moja vijana kutoka katika shule mbalimbali za Jumuiya za  Mangunze, Manjacaze, Chongoene e Xai Xai waliunganika pamoja kutafakari masuala yanayowahangaisha zaidi, hasa kama ya madawa ya kulevya, ukosefu wa usafiri kuwafikisha mashuleni, unyanyasaji wa kijinsia na utoro wa walimu. Wamesindikizwa na kikundi cha kimataifa cha Scholas na watu mahalia wa kujitolea walio andaliwa miezi ya hivi karibuni nchini Argentina. 

wanafunzi hao waliwasilisha mapendekezo yao  wakati wa  hitimisho ya kazi ya Mkutano wao mbele viongozi wa serikali mahalia wakiwepo Gavana, Alberto Zeca; , Msimamizi wa wilaya Chongoene Carlos Buchili, Mkaguzi wa Elimu wa Wilaya Francisco Machava, kamanda wa Polisi wa  wilaya Chongoene José Ernesto Divis , Kiongozi mkuu wa eneo hilo la  Conceicao, Bw.Samuel Jose Chitambo na Paroko, Padre  Juan Gabriel Arias.
Wanafunzi waliwaeleza vikwazo vikubwa wanavyokubana navyo kila siku; kwani wengi wao wanalazimika kutembea kila siku kati ya km 5 na 10 kwenda tu na hivyo pia kurudi ili kufika shuleni kwao kutoka katika vijiji na vitongoji vyao.Kutokana na hilo, wanafunzi wanaomba usafiri wa kwenda na kurudi nyumbani kwao, wakati huohuo wameomba pia uboreshaji wa  njia za ufundishaji katika mafunzo ya walimu, bila kubaguliwa kwa upande wa wale wanao kuwa wa mwisho, aidha uboreshaji wa miundo mbinu na vifaa.

Halikadhalika vijana wameonesha bayana  uwepo wa vibanda haramu karibu na shuleni kwao vinavyo uza madawa ya kulevya na pombe. Katika suala hili vijana wanatoa wito uwepo wa mpango wa sheria inayo zuia ujenzi wa vibanda  karibu na maeneo ya shule.
Kijana wa Umri wa miaka 17 kutoka katika Shule ya Sekondari ya Dambine 2000 ameeleze kwa shahuku  juu ya mkutano hu. Scholas ni sehemu muhimu ya mkutano kwa vijana , kwa sababu ya kutoa  fursa ya uwezekano wa kujadiliana matatizo yanayo wahangaisha katika jumuiya zao, shuleni kwao  na katika familia zao. Hii inatia moyo jinsi gani katika maisha yao ya kila siku wanaweza kujikimu  na kujiendeleza katika jumuiya zao kwa kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya kupinga na kudhibiti matatizo ya ulevi, madawa ya kulevya vurugu na aina nyingine za matatizo.

Wakati wa kazi yao wamejikita zaidi vijana kutafuta ushauri kwa wataalamu na wawakilishi wa jumuiya zao wali wasinidkiza katika wiki nzima. Kazi ya walimu na wataalamu hawa imekuwa muhimu sana kutokana na lengo la kukuza program hizi katika malengo ya kuhamasisha mikutano kati ya vijana lakini pia kuwapa sauti kwani watakuwa na fursa ya kutoa madai yao na mapendikezo ya kuboresha ndani ya jamii zao pia mwendelezo wa umoja.  
Walimu walikubaliana kuwa aina hii ya mikutano ya kuwaunganisha vijana ni msaada na wenye thamani ya aina yake. Kwa njia hiyo unaweza kuhakiki kwa mara nyingine wito na ujumbe wa  ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko anaye weka wazi juu ya maendeleo na mabadiliko ya hali halisi ya kijamii kwamnza yaanzie katika elimu. Timu ya Scholas kimataifa kwa siku chache za hivi karibuni itaacha nchi ya Msumbiji , lakini itakuwa imepanda mbegu ya matumaini  kwa vijana 180 ambao wanaweza kubadili mtazamo wa jamii husika.

Scholas Occurrentes ni Taasisi ya Kipapa yenye kuwa na  lengo la kuhamasisha na  kutetea, kwa njia ya elimu, sanaa na michezo, utamaduni wa kukutana kati ya vijana wa dini zote, ili kuchangia katika ujenzi wa jamii bora kupitia nguzo ya  mazungumzo  katika kuhakikisha amani duniani. Leo hii Scholas Occurrentes  imeshasimika mizizi katika nchi 190 duniani kote, ikiwa na  mtandao zaidi ya mashule 446,000 na mitandao ya kielimu  kwa madhehebu yote ya dini, umma na binafsi. Tangu Juni 2017 imekuwa na makao yake makuu katika mji wa Vatican.

 Sr Angela rwezaula
Idhaa ya kiswahili ya Radio Vatican

 

10/08/2017 16:08