2017-08-10 15:17:00

Ni vigumu kufanya mazungumzo na watu wenye mawazo na malengo tofauti


Tukiwa  wakristo tunalazimika  kutembea katika njia ya amani na kujibidisha katika kujielimisha kwenye tamaduni zote, kutokana na kuashiria  kwa hatari za kinyuklia pia kuwa na utashi wa kutaka kuondoa kabisa silaha za kinyuklia. Ni maneno ya Askofu Mkuu Silvano Tomas mwakilishi wa Vatican katika Baraza la kudumu kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva. Ameyasema hayo akitafakari juu ya maneno yanayozidi  kuleta wasaiwasi kutoka katika vyombo vya habari siku hizi kuhusu  nchi ya Marekani na Korea ya Kaskazini. Ni hali ambayo pia Baba Mtakatifu Francisko anafuatilia matukio ya hatari ya kinyuklia kutokana na kwamba  yeye tayari ameongea  wazi juu ya biashara ya silaha na kuzuia nguvu hiyo kwa njia ya kutafuta mwafaka wa majadiliano. Amejaribu kila wakati kusisitiza Jumuiya za Kimataifa kujihusisha katika kuzuia mambo yasiyokua manufaa kwa kutafuta namna ya kuzuia nguvu na migogoro. 

Ikumbukwe Rais Trump wa Marekana anatishia mashambulizi ya makali dhidi ya Rais Pyongyang wa Korea ya Kaskazini ambaye naye anajigamba kuwa na uwezo wa kuangamiza Marekani katika kambi za  Guam, kwa makombora ya kinyuklia ambayo anaendelea kusimamia kwa lengo hilo. Kwa njia hiyo Askofu Mkuu Tomas anasema kwa upande wake  iwapo sehemu hizo mbili hawakubali kuharibu na kutokutumia silaha za kinyuklia, kwa upande mwingine ni hatari na moto kwa watu wa nchi nyingine ambao pia baadhi wanafikiria kufuata nyayo za kutafuta nguvu za nyuklia za kujilinda. Kwa njia hiyo Askofu Mkuu anasisitiza ni  jinsi gani silaha za namna hiyo zina  uharibifu mkubwa kwa wakati mmoja akikumbuka uzoefu wa Vita ya Pili ya dunia, ambayo anasema ni mfano mmojawapo usio kubalika kamwe.

Anatoa wito  na ulazima wa Jumuiya zote za Kimataifa kuingilia kati ili kuhakikisha kwamba haki za binadamu zinalindwa . Hata hivyo naweka bayana kwa mara nyingine tena kuwa ni lazima kuendeleza mbele kazi ya mpango huo nyeti wa majadiliano. Hiyo ni kwasababu ya kufikiria uzoefu wa shughuli zake anazozifanya katika ofisi ya Umoja wa mataifa mjini Geneva, na kusema,anakubali kabisa  ugumu uliopo wa kuwaunganisha watu pamoja  katika meza moja wenye malengo tofauti ya kisaisa na kijeshi. “Katika meza moja ya  kuzungumza na watu wenye mawazo tofauti , malengo tofauti ya kisiasa ni vugumu sana lakini  hatupaswi kuacha kujaribu  kufanya mazungumzo  kwa njia ya ushirikiano ,kwa njia ya ushawishi, kuhusisha nchi hizo  na kuwaonesha faida ya biashara ya kimataifa, uwezekano wa maendeleo ya mali kwa ajili ya mema ya watu wao, ili weweze  kujisikia kuwa ni sehemu ya mali ya familia ya binadamu, kwa kufanya hivyo inawezekana wasijihisi haja ya kujificha nyuma ya vitisho vya nguvu”.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.