Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa Barani Afrika \ Maendeleo

Askofu Mkuu Lukudu wa Sudan kufungua ofisi za Caritas Internationalis

Askofu Lukudu wa Sudan kufungua ofisi za Caritas Internationalis zilizojengwa kwa msaada wa Shirika hilo kwa malengo ya kusaidia binadamu - REUTERS

10/08/2017 15:53

Hivi karibuni huko Juba nchini Sudan ya  Kusini wamefungua ofisi mpya za Caritas Internationalsi, ofisi ambayo itaweza kusaidia dharura katika hali za kibinadamu. Ni majengo mawili ya Caritasa ambayo yamefunguliwa na Askofu Mkuu wa Juba Paulino Lukudu  mjini Sudan ya Kusini.
Katika hotuba yake, akiwaelekea  wahudumu wa Caritas mahalia, amewatia moyo katika huduma yao wanayoitoa  pia kuonesha umuhimu wa huduma yao kuwa ni kwa ajili ya nchi yao na katika dunia. Kwa maneno hayo amewataka wafanye kazi kwa shahuku na juhudi za kuboresha nchi; kwa kushirikiana na Kanisa ambalo amesema lina jukumu kubwa la utoaji wa huduma  ya idadi ya watu.

Ikumbukwe, mwaka huu tarehe 26 Februari, Baba Mtakatifu Francisko alipotembelea Kanisa la Kiangilikan mjini Roma alikuwa ameonesha hamu ya kutembelea nchi ya Sudan ya Kisini akiwa pamoja na Askofu wa Kianglikan Justin Welby. Lakini Safari hiyo haitafanyika mwaka 2017 kwasababu bado iko katika hoja , lakini wakati huo huo Papa hajasahau nchi  hiyo ambayo tangu 2013 imeharibiwa na vita kati ya viongozi wa kisiasa. Kwa njia hiyo, mwezi wa Juni 2017, Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya huduma na maendeleo ya Binadamu  aliwasilisha katika vyombo vya habari Mpango wa Baba Mtakatifu wa kusaidia Sudan ya Kisini hasa katika sekta  ya Afya, elimu na shughuli za kilimo kwa kiasai cha  jumla karibia nusu milioni ya dola za kimarekani  ambazo Baba Mtakatifu Francisko ameamua kuonesha upendo wake na ukaribu wa taifa hilo la Sudan ya Kusini barani Afrika.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 

 

10/08/2017 15:53