Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Katekesi siku ya Jumatano

Yesu alitundikwa msalabani kwa kosa la kusamehe dhambi!

Mwenye kusamehe kidogo, hupenda kidogo.”Basi, Yesu akamwambia yule mwanamke, “Umesamehewa dhambi zako" - AP

09/08/2017 15:03

Katika Katekesi ya Baba Mtakatifu ya kila Jumatano mjini Vatican, hata leo tarehe 9 Agosti 2017 ameendelea na Katekesi yake katika Ukumbi wa Mwenye Heri Paulo VI. Katekesi yake imegusia kuhusu msamaha wa Mungu ni kama injini ya matumaini.Tafakari yake  imetokana na Injili ya Mtakatifu Luka kuhusu mwanamke aliye mnawisha miguu Yesu kwenye nyumba ya Simon aliyokuwa amekaribishwa, hivyo ndipo Yesu  “akamgeukia yule mwanamke na kumwambia Simoni, “Unamwona huyu mwanamke, sivyo?. Basi, mimi nilipoingia hapa nyumbani kwako hukunipa maji ya kunawa miguu yangu; lakini mwanamke huyu ameniosha miguu yangu kwa machozi yake na kunipangusa kwa nywele zake. Kwa hiyo nakwambia amesamehewa dhambi zake nyingi kwa kuwa ameonyesha upendo mkubwa. Mwenye kusamehe kidogo, hupenda kidogo.”basi, Yesu akamwambia yule mwanamke, “umesamehewa dhambi zako.” Na hapo wale waliokuwa pamoja naye mezani wakaulizana, “Ni mtu wa namna gani huyu awezaye kusamehe dhambi?” Naye Yesu akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”

Baba Mtakatifu Francisko ameanza akisema kuwa wamemsikiliza  Mfarisayo Simoni akisema ni nani huyo anaye samehe dhambi (Lk 7,49). Hiyo nikutokana na kwamba Yesu amemamaliza kutenda jambola aibu . Kwani Mwamke huyo katika mji alijulikana mwenye dambi na akaingia masikini akiwa amejificha  katika nyumba ya Simoni, alitaka asijulikane ili asije akauwawa kama ilivyokuwa kasumba ya wakati huo. Aliinamia miguu ya Yesu una kunawisha na baadaye akampaka mafuta ya kunukia. Wote ndani walianza kunung’unika wakisema Kama Yesu angekuwa ni Nabii  asingekubali kufanyiwa ishara ya namna hii ya mwanamke kama huyo. Katika mantiki ya wakati Baba Mtakatifu Francisko anafafanua, kati ya mtakatifu , mwenye dhambi , kati ya msafi na mchafu , ubaguzi ulikuwa lazima ufanyike kwa hakika.

Lakini kwa mantiki ya Yesu mtazamo wake  ulikuwa tofauti. Tangu mwanzo wa utume wake huko Galilaya, yeye aliwakaribia wakoma, wanye mapepo wabaya, wagonjwa na waliobaguliwa. Tabia ya namna hiyo haikuwa ya kawaida, kwani tabia ya Yesu mbele ya uchungu huo uliamsha hisia ya  moyo wake wenye upendo mkuu kuwakaribia na kuwapenda watu walio baguliwa na wasioguswa ambapo baadaye ukaleta  mafarakano kati ya watu wake.
Pale ambapo kuna mateso, ndipo Yesu anakuwapo,hubeba hayo matatizo, na mateso  hayo yanakuwa ya kwake anasema Baba Mtakatifu.Yesu hakuhubiri kwamba hali ya mateso inapaswa kuvumiliwa kwa ujasiri, kama  vile ya wataalamu wa filosofia ya wakati ule. Yesu anashiriki mateso ya binadamu anapokumbana nayo  ndani ya moyo wake na ndiyo tabia ya kikristo: katika huruma,Yesu anafanya uzoefu wa mateso.Kwa maana nyingine Yesu anasikia mateso ndani ya mwiliwa wake. Ni mara ngapi katika Injili tunakutana  hali ya namna hiyo. Moyo wa Yesu unatwaa na  kuonesha moyo wa Mungu , mahali ambapo kuna binadamu, mke na mme anayeteseka na kutaka kuponywa, kukombolewa  mateso yake.

Kwa njia hiyo Yesu anafungua mikono yake kwa ajili ya wadhambi. Ni watu wangapi waddhambi  hata leo wanaendelea katika maisha yaliyokosewa  , na hawana mtu wa kuwa tayari kuwatazama au kuwatazama kwa namna tofauti  yaani , kwa macho yenye huruma, au  kusema zaidi kwa moyo wa Mungu maana yake  kwa  matumaini. Yesu mwenyee anaona huo uwezekano  wa kufufuka hata katika uchanguzi mwingi wa makosa au kuosea njia.
Baba Mtakatifu ameonesha akisema, mara nyingi ipo hali ya  kusahau kwamba ,Yesu aliingia katika upendo usio rahisi, na usiyo kuwa na faida. Injili zinaonesha, matukio hasi juu ya Yesu  na hasa pale anapo samehe dhambi  kwa mfano wa mwanaume aliyekuwa amepooza (Mk 2,1-12). Ni mwanaume aliyekuwa anateseka  mara mbili kwasababu alikuwa hawezi kusimama na alikuwa anajisikia mwenye dhambi. Yesu alitambua uchungu wake jinsi ulivyo kuwa mkubwa na ndiyo maana alimkaribisha na kumponya akisema mwanangu umesamehewa dhambi zako. Baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wameketi hapo wakawaza mioyoni mwao  kuwa amekufuru, kwasababu hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake .

Anasisitiza Baba Mtakatifu akisema, sisi tuliozoea kufanya uzoefu wa msamaha wa dhambi, labda hata kuzidi kiasi, tunapaswa wakat mwingine kukumbuka jinsi gani upendo wa Mungu ulivyonunuliwa kwa gharam kubwa. Yesu hakubambwa  msalabani kwasababu ya wagonjwa kupona, kwasababu ya kuhubiri upendo au  kwasababu ya kutangaza heri . Mwana wa Mungu anatundikwa msalabani kwasababu amesamehe dhambi, kwasababu anataka uhuru wa kamili wa moyo wa binadamu.Yesu hakubali kwamba binadamu amalizie maisha yake yote  akiwa na chale isiyofutika katika mawazo ya kutokuweza kupokea ndani ya moyo wake ile huruma ya Mungu. Kwa njia hiyo wadhambi wanasamehewa, na siyo tu kutulizwa kwa tabia za  kisaikolija , kama sababu ya kuwa huru kwa mantiki ya dhambi. Yesu anafanya zaidi ya limu ya saikolojia  maana anatoa fursa ya mtu aliye kosea kuwa na matumaini, pia kuwa kiumbe kipya, yaani maisha yanayojikita ndani ya upendo. Matayo mtoza ushuru aligeuka kawa mtume wa Kristo. Zakayo mtoza ushuru na tajiri huko Yeriko alibadilika  akawa mfadhiri wa masikini, Mwanamke msamaria aliyeolewa na wanaume watano,wakati huo alikuwa akiishi na mwingine asiye wa kwake,aliahidiwa chemichemi ya maji ya uhai  wenye maisha ya milele (Gv 4,14).

Baba Mtakatifu Francisko amemalizia katekesi yake  akisema ni vizuri kufikiria kwamba Mungu hakuchagua kufinyanga na kutengeneza Kanisa na kuliweka  juu ya watu wasio kosea kamwe. Kanisa ni watu wadhambi ambao lakini  wanafanya uzoefu wa huruma na msamaha wa Mungu . Petro alitambua ukweli mwenyewe baada ya jogoo kuwika. Pamoja na ukarimu wake na mambo mengi yaliyokuwa yakimvimbisha kifua  kwa kujisikia yeye kuwa zaidi ya watu wengine. Wote ni tu masikini wadhambi ni wahitaji wa huruma ya Mungu mwenye kuw na nguvu ya kutubadili, na kutupatia matumaini kila siku. Watu waliotambua ukweli huo msingi Mungu anawapatia utume mzuri duniani. Kwa maana ya kusema upendo kwa ndugu kaka na dada, na kutangaza huruma ya kwamba Mungu hamkani hata mmoja. Na hiyo ndiyo matumani,  hivyo basi tuendelee mbele na matumaini hayo ya msamaha, katika upendo na huruma ya Yesu.

Mara baada ya katekesi yake kama kawaida amewasalimia mahujaji wote walio fika katika ukumbi , wakati huo huo na vijana akisema  wanaotembelea katika sehemu za utamadnui kama vile  sanaa, na kwamba iwe kwao fursa ya kutambua na kufuata nyayo kwa mifanoiliyo achwa  na mashuhuda wengi wa Injili kama vile Mtakatifu Laurent ambaye tarehe 10 Agosti kanisa linamkubuka. Anawatia moyo wagonjwa wote waungane kila wakati na mateso ya Yesu wakibeba msalaba kwa imani ya ukombozi wa dunia. Aidha wenye ndoa wapya ambao hawakosi kila wakati katika katekesi yake  Baba Mtakatifu amewatakia familia zao mpya ziwe na imani ya Injili na katika upendo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili

09/08/2017 15:03