2017-08-08 16:30:00

Colombia:Papa mjumbe wa furaha anaanguka kama mvua katika jangwa


“Ni mjumbe aliyejaa furaha katumwa  na Bwana. Anakuja kama mvua katika jangwa ili kuleta matumaini kwa watu wetu”. Ndiyo maneno ya mwanzo wa wimbo rasmi uliotungwa kwa ajili ya mapokezi ya ziara ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Colombia . Ziara ya Baba Mtakatifu inatarajiwa mwezi ujao kuanzia tarehe 6 hadi 10 ambapo tarehe 11 Septemba 2017atarudi na kutua uwanja mdogo wa ndege Ciampino  nchini Italia . Kauli mbiu  iliyochaguliwa katika ziara yake ya kitume ni ”tufanye hatua ya kwanza” . Baba Mtakatifu anafika nchini Colombia  kuenzi mchakato wa maridhiano  katika nchi ambayo kwa miaka 50 wamekuwa katika vita ya wao kwa wao kati ya serikali ya Bogota na Farc (Fuerzas Armadas Revolucionarias de Colombia).

”Baba Mtakatifu anakuja mwisho wa mchakato wa safari ya Colombia”. Hayo ni maneno ya Padre Francisko Bortignon , Paroko wa Cúcuta Kaskazini ya nchi ya Colombia , parokia inayo pakana na nchi ya Venezuela. Yeye ni mmisionari  wa Shirika la Wascalabriani ambapo kwa miaka 21 yuko nchini Colombia, lakini mzaliwa wa Mkoa wa Veneto nchini Italia na ni mkurugenzi wa kituo cha wahamiaji na mapokezi hapo Cucuta. Katika kituo cha wahamiaji wanawapokea watu wengi na hasa zaidi ni kutoka nchi ya Venezuela wanaotafuta mahali pa kukumbilia kutokana na migogoro ya vurugu, njaa na umasikini nchini mwao inayoendela kuwa tishio.

Katika maongezi yake kwa njia ya simu ameelezea juu ya hali hasi ya nchi ya Colombia ambayo kwasasa anasema wameweza kutia sahini ya makubaliano ya amani baada ya mapigano ya muda mrefu na kikundi cha Farc.  Lakini pamoja na hayo bado wamekebaki vikundi vidogovidogo kama vile Eln na majeshi ya taifa ya kudai huru. Anaongeza kusema, hawa bado wako katika mchakato kwasababu mchakato huo unakwenda polepole lakini wenye kuwa na matumaini ya kwamba kufikia miaka miwili wanaweza kufikia lengo kubwa na kusahini makubaliano ya amani. Anaongeza, ni kwa njia hiyo tu ndipo serikali inaweza kufikia utulivu muhimu wa kusitisha mapigano hayo. Na hiyo ingemaanisha zaidi usalama na matumaini ya kukua kwa uchumi na maendeleo.

Kanisa Katoliki la Colombia daima limefaya kazi ili kufikia amani, Padre Francesco Bortignon, anasema; hadi sasa wanaendelea kwa nguvu zote kuhamasisha na  kuwasindikiza katika mchakato wa amani. Makanisa mengi na hasa yale yaliyoshambuliwa na wanamgambo  wanandelea kuanzisha nguvu zao za mshikamano kijamii kupanga na kuwaandaa viongozi, pia katika shughuli za ujasiliamali na  kwa namna ya kuandaa kiakili na kidhamiri kwa namna  ya kujiandaa katika maisha ya kidemokrasia, ushirikiano na uzalishaji.

Ujumbe ambao Baba Mtakatifu atakao ukuta katika ziara yake ni ule kweli wa Kikristo na kiinjili. Ni ujumbe wa matumani, ni ujume wa safari ndefu ya ushuhuda wa kikristo kwa dhati; na ndiyo maana ya kauli mbiu isemayo tufanye hatua ya kwanza. Hiyo ni muhimu sana hasa kwa nyakati hizi; anamaliza Padre Bortignon, katika nchi ya Colombia mahali ambapo kumeibuka matukio mengi ya  madhehebu kama uyoga na isitoshe hadi kufikia hali za watu kufikiria uchawi,na kujiingiza katika waganga wa kienyeji.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.