2017-08-08 16:17:00

Baba Mtakatifu amemteua Askofu msaidizi wa Jimbo la Philadelphia


Baba Mtakatifu Francisko wamemteu  Askofu msaidizi wa Philadelfia ya Ucraine(USA) Padre  Andriy Rabiy. Askofu mteule  Adriy Rabiy alizaliwa huko  Lviv nchini Ukraine tarehe 1 Oktoba 1975. Alihamia nchini Marekani na wazazidi wake  na kuishi huko. Alipokea majiundo ya upadre katika Seminari ya Kiukraine ya Mtakatifu Josaphat Washington DC. Mwaka 1998 aliendelea na masomo ya Filosofia katika Chuo  Kikuu katolikicha Marekani. Mwaka 2002 akapata Master ya  Taalimungu katika Chuo cha Kitaali Mungu cha mapadre wa Kidomenican huko Washington DC. Mwaka 2008 akapata shahada ya Sheria kwenye Chuo Kikuu Katoliki nchini Marekani.

Alipata daraja la ushemasi tarehe 15 Novemba 1998 na upadrisho tarehe 19 Desemba 2001. Kwa sasa alikuwa akiendelea na utume  kichungaji katika Jimbo la Piladelphia ya Ucraine nchini Marekani na pia kuwa na nyadhifa mbalimbali za kijimbo zikiwemo pia kuwa mmojawapo katika Baraza la ushauri na uendeshaji wa Baraza  Maaskofu Katoliki wa Pennsylvania, pia Mkurugenzi wa Kituo cha  kutetea na kulinda  watoto na vijana


Na pia Baraza la Maaskofu wa Marekani ya (USCCB) wametenga kiasi cha Milioni 4 za dola ya Kimarekani kwa ajili ya kusaidia kazi za kichungaji katika Makanisa ya Mashariki ya Kusini na visiwa vya Karibean, na karibia milioni 2 za dola ya kimarekani kwa aajili ya kujenzi wa Kisiwa cha Haiti. Mpango wa Haiti unatazama kushughulikia vituo 400 vya mafunzo kichungaji kwenye Parokia nne zilizoa haribiwa na kimbunga (Matthew).Huu ni msaada wa kwanza kutolewa kwa ajili ya kuwasaidia makanisa ya mashariki ya Haiti baada ya mahafa makubwa ya mafuriko.

Wameshangazwa na ukarimu wa wakatoliki wa Marekani,  kutokana na kwamba, kutakuwa na utofauti wa maisha ya watu wengi wa Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribean. Ni maneno ya Rais wa Tume ya Kanisa la Amerika ya Kusini na wa Baraza la maaskofu wa Marekani ,Elizondo, ambaye ni Askofu Msaidizi wa Jimbo la Seattle. Ukarimu huo unaonesha upendo na huruma ya Mungu. Ameongeza kusema, anaona jibu ambalo wamepokea kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko. Kwa msaada huu na siyo tu kwa ajili ya kuanzisha miradi kichungaji bali hata kuweza kujenga makanisa mbalimbali ya Majimbo ya Haiti. Baada ya tetemeko la Ardhi mwaka 2010; Baraza la Maaskofu wa Marekani walianzisha kampeni nyingi za kuhamasisha kusaidia Haiti.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.