Inasemekana waathirika 11 na majeruhi wasio kuwa na idadi katokana na shambulizi la Kanisa la Mtakatifu Filippo huko Ozubulu Kusini Mashariki mwa Nigeria Jumapili asubuhi ya tarehe 6 Agosti 2017. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari mahalia na Polisi wanasema mtu mmoja aliingia Kanisani wakati watu wanasali na kuanza kushambulia kwa kuwapiga risasi hovyo. Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Jose na amabaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Nigeria Ignatius Kaigama , ameelezea masikitiko yake akiwa nchini Italia. Anasema, ametafuta namna ya kuwasiliana na Maaskofu mahalia ili kupata habari kamili juu ya tukio hilo mara baada ya kupokea habari hizo.
Katika maelezo yake anasema hawajuhi sababu ya vitendo hivyo visivyo vya kibinadamu; aidha, siyo rahisi kabisa kufikiria kitendo cha namna hiyo dhidi ya watu wasio kuwa na hatia wakiwa Kanisani saa kumi mbili za alfajiri wakisali. Kwa mujibu wa uchunguzi, inasemekana sababu za tukio hilo likawa wahusiaka ni makabila kulipiza visasi na wala siyo tendo la kigaidi. Hii ni kutokana na kwamba eneo la mashambulizi yaliyotokea siyo eneo la kutishwa na kukundi cha kiislam wa Boko Haram, ambao wamekwisha fanya mashambulizi kadhaa dhidi ya wakristo na hata waislam katika maeneo ya Kaskazini mashariki ya nchi hiyo. Jimbo la Nnewi ambalo ndimo Parokia ya Ozubulu iko Katika Serikali ya Kusini mwa Nigeria mahali ambapo wakristo ndiyo walio wengi.
Askofu Mkuu Kaigama ameeleza kuwa eneo hilo limejaa wakristo kwa wingi kwa maana
ya kwamba ukatoliki katika eneo hilo umesimika mizizi kwa muda mrefu. Wamisionari
wa kwanza walifika eneo hilo mwaka 1885. Kutokana na uzoefu wake ni kwamba eneo hilo
linaweza kuonekana matukio ya vurugu za kijamii, hasa zinazohusiana na ardhi katika
masuala ya kilimo, lakini mashambulizi ndani ya Kanisa limekuwa ni tukio lisilotarajiwa
kabisa.
Kwa njia hiyo Askofu Mkuu Kaigama anaomba, tukio hili la kigaidi liwe la kipekee na
lisihusishwe na ugaidi, kwani anaongeza;Nigeria wamepata matatizo mengine na hawataki
tena mivutano hiyo ikue. Wanahitaji amani kwasababu nchi yao ni yenye rasilimali nyingi
ambazo zikitumika vizuri zitawaruhusu kuishi kwa amani.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |