2017-08-07 16:31:00

Baba Mtakatifu awataka watu wa Peru kufanya kazi kwa ajili ya umoja


Fanyeni kazi kwa ajili ya umoja, huo ndiyo wito wa Baba Mtakatifu Francisko ameutoa kwa watu wote wa  nchi ya Peru ikiwa ni katika maandalizi ya ziara yake ya Kitume nchini humo inayotarajiwa kufanyika  mwezi Januari 2018.  Wito huo umetolewa kwa njia ya video  ambapo  Kardinali Juan Luis Ciprian Thorne Askofu Mkuu wa Lima ameuwezesha usikike kwa watu wote. Baba Mtakatifu Francisko katika maelezo yake anaonesha shahuku yake ya kuelekea nchi hiyo ya Amerika ya Kusini mahali ambapo amesema  wana utajiri wa mali ya asili. Amesema mali asili na nzuri ambayo anaweza kuwa nayo baba ni ile ya watakatifu. Hiyo ni kwasababu nchi ya Peru ina watakatifu wengi katika Bara la Amerika ya Kusini. Hawa ni wajenzi wa Kanisa ambao wameijenga njia na kujionesha  katika umoja; na mtakatifu anafanya kazi daima katika njia hiyo kwa malengo  daima ya umoja .Hilo ndilo jambo ambalo Yesu alifanya, mkristo ahana budi kufuata nyayo hiyo.

Kutokana na hayo Baba Mtakatifu anawalika watu wa nchi ya Peru kutembea kwa pamoja katika njia ya watakatifu wengi  nchini humo na kufanya kazi kwa ajili ya umoja. Anayefanya kazi ya kwa ajili ya umoja daima utazama mbele , aidha anauliza swali je inawezekana kutazama mbele ukiwa mwenye shingo ngumu na uchungu. Hapana kwasababu mkristo anatazama mbele kwa matumaini , anategemea kufikia kile ambacho Bwana aliahidi. Kwa namna hiyo wafanye kazi kwa ajili ya umoja na juu ya matumaini.
Kwa maneno hayo amewasalimia watu wote nchini Peru akiwapa ahadi ya kukutana nao katika tarajio la  ziara ya kitume  ijayo. Ziara nchini Peru inategemea kufanyika kuanzia tarehe 15 hadi 21 Januari 2018 na atatembelea mji wa Lima , Puerto Maldonado na Trujillo.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.