Taarifa kutoka katika Shirika la habari Katoliki la CAN linasema, Waziri wa mawasiliano na tekenolojia amepongeza vyombo Katoliki vya Habari katika nchi mapema wiki hii kwa jitihada zao za uinjilishaji ikiwa ni pamoja na kuadhimisha siku ya 51 ya Mawasiliano duniani. Waziri wa habari Nicholas Daus amesema mkatoliki anaongeza msaada kwa Kanisa. Ameyasema hayo baada ya kutembelea ofisi ya Radio FM Tuntufye katika kituo kilichopo Jimboni Karonga. Vilevile akizungumza na vyombo vya habari Katoliki katika Parokia ya Mtakatifu Maria huko Karonga amewahimiza wasikatishwe tamaa na upungufu wa masafa katika huduma yao. Aidha wawe makini,wasifurahishwe hata kidogo habari mbaya au kitu ambacho kinaweza kuwadhuru wengine. Amesema kwa kutumia chombo cha habari cha Kanisa ni muhimu kuendesha utume wa uinjilishaji. Amewasifu vikundi vya wanahabari na kuthibitisha juu ya utoaji wa msaada wa serikali, na kwamba anavutiwa jinsi gani Tuntufye FM katika Jimbo la Karonga inavyofanya kazi vizuri.
Naye Askofu Martin Mtumbuka wa Jimbo la Karonga nchini Malawi wakati wa kuadhimisha Misa Takatifu katika mahubiri yake amesema mambo yote mawili yanatoa changamoto na akatoa shukrani kwa wale wote waliokusanyika. Pamoja na hayo amechangamotisha nyumba za vyombo vya habari zao na wale wanaofanya kazi katika vyombo hivyo kwamba angependelea vyombo hivyo viwe vya kitaalam na pia wafanyakazi wawe wataalamu zaidi. Hata hivyo amemshukuru Mungu kwa zawadi ya vyombo vyote vya mawasiliano, pamoja na kwamba amesema, changamoto ni kwao binafsi ya kuweza kuzitumia kwa ufanisi. Ameongeza kusema inawezekana kufanya vizuri zaidi kuliko kile kinachofanyika katika vituo vya televisheni, redio na magazeti.
Askofu aliongeza kusema,"Hebu tutoe ujumbe wa imani kwa ajili ya utukufu wa Mungu
na maendeleo ya taifa hili”.Sisi ndiyo wanaopigania hii, hii inaweza kufanyika kulingana
na msingi wa jinsi gani tunavyofanya mambo. Hebu tufanye mambo kwa njia ya kuratibu
na kuwa na ubunifu”Amesema.
Katika maadhimisho hayo pia Askofu George Tambala wa Zomba ambaye ni Rais wa mawasiliano
wa Baraza la maaskofu nchini Malawi, alitafakari kuhusu ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko
wa Siku ya Mawasiliano ya 51 Duniani akisema, Baba Mtakatifu Francisko anatuhimiza
sote kuvunjavunja mduara wa wasiwasi na kuongeza hofu ambayo husababishwa kukazia
mara kwa mara habari mbaya kama vile vita, ugaidi, kashfa na kila aina ya kushindwa
kwa binadamu.
Aidha amebainisha kuwa ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko unachangamotisha kwamba waandishi wote wa vyombo vya habari wanapaswa kutafuta njia ya wazi,ya ubunifu ya mawasiliano ambayo haitukuzi uovu lakini badala yake ni kuzingatia ufumbuzi na kuhamasisha njia nzuri na pendelevu kwa upande wa mpokeaji wa habari hiyo. Vyombo vya habari Katoliki nchini Malawi vinajumuisha tume ya Maaskofu ya mawasiliano ya kijamii kama vile Radio Maria Malawi; Radio Alinafe; Tigabane ; Tuntufye FM; Televisheni ya Luntha, Montfort na Gazeti la Likuni.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |