2017-08-04 16:02:00

Vatican yatoa mchango kwa ajili wajane na watoto yatima Nigeria


Ni karibia wanawake 5 elfu wajane walio achwa na waume zao baada ya kuwawa kikundi cha wanamgambo wa kiislam wa Boko haramu walioko Kaskazin ya  chini ya  Nigeria  hasa katika mikoa ya Bono, Yobe na Adanwa. Wanamgambo hao wameshambulia maeneo yote hayo ya Kaskazini kwa kipindi cha muda mrefu na hasa  maeneo yote ya jimbo la Maiduguri. Baada ya  makala ya jimbo inayo ongozwa na Monsinyo Oliver Dashe Doeme, Shirika la Kipapa kwa ajili ya Kanisa hitaji wamemeamua kusaidia wanawake hawa na watoto yatima kwa kutoa mchango wa euro 70 elfu zitakazoweza kusaidia Chama cha Mtakatifu Judith Mjane. Ni Chama kilichoanzishwa kwa  kwa utashi wa Askofu wa Jimbo la Maiduguri.

Mpango huo una lengo la kutazama mahitaji yote ya wanawake, anaeleleza mkurugenzi wa Shirika la kipapa la kusaidia Kanisa hitaji kwa upande wa Jimbo la Maiduguri . Pamoja na hayo ni kuwapa mahitaji ya kuweza kuishi maelfu ya watoto yatima walio baki kutokana wazazi kuwawa na ukatili wa kikundi cha Boko Haram. Msaada huo utawawezesha wanwawake wajane na watoto wao pia watoto hao  kuendelea na mafunzo shuleni.
Kwa mujibu wa Baraza  la Kipapa kwa ajili ya Kanisa hitaji limeonesha kuwa hadi sasa nchini Nigeria ni zaidi ya waathirika 20 elfu kutokana na vitendo viovu vya waalifu. Aidha wanasema vitendo hivyo vya vurugu, ghasia na mahuaji  vimesababisha  karibu milioni 26 ya watu wa Nigeria na  milioni 2.3 ya watoto kukosa kwenda mashule.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.