Tuiombee nchi Takatifu: siyo mbali na eneo waliokuta masalia ya Mtakatifu Stefano
ambaye ni msimamizi wa nchi hii; eneo hili ni maarufu katika kusikitisha maana kuna
ukuta wa kutenganisha nchi. Ni utumbuzi muhimu wa wayahudi na warabu ambao kwa pamoja
wanaitwa kushirikishana huruma ya Mungu mwenye nguvu na uweza pia ulazima wa kujishinda
wenyewe ili kujenga na kulinda mioyo kwa ajili ya kupata amani ya kweli na yenye
kudumu.
Haya ni maneno ya Kardinali Leonardi Sandri Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya
makanisa ya Mashariki Alhamis, tarehe 3 Agosti 2017 wakati wa maadhimisho ya misa
ya kipapa katika Sikukuu ya msimamizi Mtakatifu Stefano shahidi kwenye Kanisa Kuu
la Mapatano.
Katika mahubiri yake Kardinali Sandri amesema, Bwana hafichi maajabu yake kwa maana
anaweza hata kuwahukumu mitume wake. Ameonesha kwamba maneno hayo katika somo hayaelezi
mambo ya kale au yaliyopitwa na wakati bali maneno ya Mungu yanaendelea hata leo
katika ulimwengu uliojaa machungu kwa namna ya pekee katika dunia ya nchi za Mashariki
ambamo ndugu na marafiki wanaishi na kuendelea kuteswa.
Kardinali Sandri akiongelea juu ya ndugu wa Iraq amekumbuka watu waliokufa akianzia
na Askofu Raho wa Mosul, Padre Ragheed Ghanni, hadi mapadre,watoto na waamini wengine
katoka Kanisa kuu Katoliki la Mama wa shauri jema huko Baghdad. Katika kutafakari
mateso makubwa ya namna hiyo anasema ni vema kuendelea mbele kwa kumtumania Mungu.
Amemalizia mahibiri yake akiomba Mungu neema ya kuwa watu wa matumaini ambao wanaonesha
mwanga na kwamba Mungu aimarishe zaidi neema hiyo ndani ya mioyo yao. Na Mama Maria
mama wa Mungu aliyeona Jumuiya ya kutume huko Yerusalem ikikua pia shahidi Mtakatifu
Stefano azidi kuwa mfano mwema wa kuigwa.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |