2017-08-04 14:45:00

Dunia iwaombee na kuwasaidia wakristo warudi katika nchi zao


Kwa miaka kumi na tano jumuiya za kikristo zilizoko hasa katika kanda ya kaskazini mwa Iraq wamepata masumbuko na mateso mengi yaliyosababishwa na ugaidi wa serikali ya kiislam (Daesh). Kutokana na madhehebu ya itikadi kali yaliyoibuka kama uyoga nchini Iraq, yamesababisha hata hali kuwa mbaya ya kisiasa na kiuchumi: kama miaka ya 90 wakristo walikuwa zaidi ya milioni moja , kwa mwaka  2006 walikuwa wakihesabiwa karibia 300 elfu tu.
Kutokana na Takwimu zilizotolewa hivi karibuni kuhusu idadi ya wakristo wa nchi za Mashariki, Patriaki wa Babilonia Luis Raphael I Sako anafikiria kwamba ulimwengu wote unapaswa kuwaombea na  kuwasaidia wakristo hao ili waweze  kubaki katika nchi zao,na kwa sasa wakristo wanakabiliwa na matatizo mengi kama vile mashambulizi ya mara kwa mara  na kuteswa.

Lakini pamoja na hayo yote wanao wito na  utume muhimu, hata wakiwa nje ya nchi wao ni lazima kuzungumzia juu ya uwepo wao kwa  kuwaonesha thamani  muhimu hata katika ulimwengu wa waislam ambao wameshindwa kutekeleza sheria za kweli za dini ya kiislam.
Kwa njia hiyo wanaweza kuwasaidia  hawa ndugu hasa magaidi kufungua mioyo yao kidogo, na kuwaleza aukuwaonesha nini dunia inahitaji,yaaani dunia inahitaji kuheshiamiana, kushirikishana na kukaribishana.

Patriaki Sako anasistiza kuwa huo ndiyo utume wa kikristo wanao paswa kuutenda kwa kila kiumbe.Pamoja na hayo Patriaki Sako anasema hali halisi ya nchi hizo lakini imekuwa kidogo afadhali kulingana na nyakati zilizopita lakini hata hivyo bado kuna woga wa nyakati zijazo,na hiyo ni kutokana na migogoro ya makundi ya magaidi wa Daesh yaani Serilaki ya kiilsam, ambayo bado hawajatoweka kabisa. Watu bado wanaogopa itikadi kali zao zenye mawazo yanayokwenda kunyume kabisa na dini ya Kiislam. Anaendelea kusema, katika kanda ya Ninawi bado kuna matatizo ya wakazi wake wakristo wanaotakiwa kurudi makwao.Tatizo kubwa hasa Serikali ya nchi haina fedha. Kanisa Katoliki limeanza kusaidia katika ujenzi wa nyumba na shahuku kubwa hipo ya wakristo kutaka kurudi katika maeneo yao, lakini pamoja na hayo bado kuna matatizo makubwa.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.