Zimesalia siku mbili za uchaguzi Mkuu wa rais nchini Rwanda na vyama tisa vinashiriki na rais Paul Kagame wa chama cha RPF. Chama cha Green Party cha Frank Habineza ndicho chama pekee halisi cha upinzani. Uchanguzi Mkuu nchini Rwanda unatarajiwa kufanyika tarehe 4 Agosti 2017. Bwana Frank Habineza amejitosa kugombea kiti cha urais kwa mara ya kwanza baada ya miaka minane ya mapambano ili kuweza kukiandikisha chama chake na kupata nafasi ya kuingizwa katika makaratasi ya kupigia kura. Frank Habineza ni mwanaharakati wa kulinda mazingira anayewania kuwa rais wa Rwanda na mwenye umri wa miaka 40. Ni kiongozi wa chama cha Green Party ambaye amekabiliana na vitisho vya kuuwawa na pia ameshuhudia wanao muunga mkono wakipigwa, wakifungwa jela na kulazimishwa kuikimbia nchini hiyo na kwenda kuishi uhamishoni wakati akijaribu kuingia katika uwanja wa kisiasa nchini Rwanda ambao una udhibiti mkubwa.
Bwanan Habineza akiongea na Shirika la habari la Ufaransa la AFP katika mahojiano kwenye ofisi yake katika mji mkuu Kigali, ambako walinzi wake wana ulizni mkali, amesema imekuwa ni safari ngumu na pia safari ya hatari. Historia fupi ya maisha yake ni kwamba, alizaliwa uhamishoni nchini Uganda baba yake akiwa ni Mhutu na mama yake Mtutsi, alirejea nchini Rwanda na kusomea masuala ya utawala. Pia alianza kuwa mwanaharakati wa asasi za kijamii , akifanya kampeni ya ulinzi wa mazingira. Habineza alikuwa mwanachama wa chama utawala cha Rwandan Patriotic Front RPF lakini akajitoa na kujiunga na siasa za upinzani mwaka 2009 ili kuweza kuwa na chama mbadala kwa chama tawala ambacho kinatawala kwas asa.
Katika kampeni za uchaguzi Rais Paul Kagame amekuwa akishutumiwa kwa kuzuwia uhuru wa kutoa mawazo na kuzuia vyama vya upinzani. Mbali na chama cha Habineza cha Green Party, hata hivyo vyama vyote vya upinzani vilivyosajiliwa vinamuunga mkono Kagame. Akiendelea na mahojiano hayo amesema walipo anzisha chama walipigwa katika baadhi ya mikutano yao na watu ambao walikuwa na silaha, watu waliwekwa maabusu,walifungwa,wengine walikimbilia uhamishoni. Chama chake kilizuiliwa usajili kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010, na muda mfupi kabla ya uchaguzi mwili wa makamu wa rais wa chama cha Green Andre Rwisereka ulipatikana ukiwa umeharibika kabisa. Habineza , ambaye anasema binafsi pia alipokea vitisho vya kuuwawa na aliamua kukimbilia nchi ya Sweden mwezi mmoja baadaye familia yake hatimaye ilipata uraia.
Historia ya mpanzani wa Rais Kagame inaendelea: mwaka 2012 aliamua kurejea nchini Rwanda. Amesema kumuacha mkewe na watoto ikiwa ni pamoja na mtoto wake wa kiume wa mwaka mmoja, ilikuwa kitu kigumu sana ambacho amewahi kufanya. Lakini Chama chake hatimaye kilifanikiwa kusajiliwa mwaka 2013, mwezi mmoja tu kabla ya uchaguzi wa bunge, ambapo Habineza aliamua kutoshiriki kutokana na ukosefu wa muda wa matayarisho. Mwaka 2015 alikuwa mgombea pekee kushiriki katika kura ya maoni ya mageuzi ya katiba inayomruhusu Kagame kuwania muhula wa tatu madarakani. Habineza alirejesha uraia wa Sweden ili kuweza kushiriki katika uchaguzi wa mwaka huu 2017 na ameendelea kukabiliana na vikwazo chungu nzima katika kila hatua. Mwaka 2016 aliotolewa kutoka katika jengo la ofisi yake na nyumbani kwake bila kupewa taarifa, aidha katika kufanya kampeni imekuwa taabu kwake.
Je atafanikiwa kupata ushindi wa kuwa rais wa Rwanda ?
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |