Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Kanisa \ Kanisa Ulimwenguni

Watu wote wasali kwa ajili ya Sudan ya Kusini ili wapate msaada

Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby akiwa anabariki Jimbo jipya wakati yuko ziarani nchini Sudan ya Kusini - REUTERS

01/08/2017 15:20

Ubinadamu mkubwa ambao nchi inataka kujaribu kufanya ni kupokea wakimbizi , historia nyingi za amani mapatano ambazo viongozi wa kikristo na waislam wanajaribu kwa njia zote kutekeleza. Haya ni mambo muhimu makuuu  ambayo yameshangaza sana Askofu Mkuu wa Canterbury  Justin Welby ambaye ni kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya kianglikan nchini Uingereza ,ambaye yuko katika  matembezi  kwenye nchi ya  Sudan,  na  siku hizii yuko katika Jimbo la Kadugli kwenye milima ya Nuba, mahali ambapo alikutana na viongozi wa madhehebu  ya kidini  pia namba kubwa ya wakimbizi ambao amepata kuwasikiliza na kuongea nao.

Katika maadishi yake Askofu Mkuu Welby  kwenye  ukurasa wa mitandao ya kijamii wa Facebook anasema 
kuwa ni fursa yake ya pekee kuitembelea nchi ya Sudan . Mambo mawili yamemshangaza, hawali ya yote ni jinsi gani nchi hiyo  wanakabiliana na wakimbizi wengi hivyo. Nchi ya Sudan ni mfano wa kuigwa na watu wengi katika dunia hii kwa ajili ya wakimbizi na wenye kuhitaji. Anaongeza kusema kuwa anaamini kwamba, kupokea wakimbizi wengi namna hii imekuwa ni changamoto kubwa na watu wa Sudan wameonesha kuwa na ubinadamu wa kweli.

Jambo la pili ambalo limestahajabisha Askofu Mkuu Welby ni matumaini ya watu wa Sudan waliyo nayo  kwa ajili ya amani na mshikamano na  ambao nchi leo hii inatarajia. Anayasema hayo kutokana na kusikiliza na kuongea na viongozi wa kikrsto na kiislam huko Madugli, na kwamba amesikia historia za watu wote wanao taka amani, ambao wako bega kwa bega wakitafuta namna ya kufikia amani hiyo ya kweli. "Nchi ya Sudan kweli inahitaji amani kwa maana inatambua zaidi ya wengine  gharama ya vita ni nini". Kwa njia hiyo Askofu Mkuu Welby  anawaalika waamini wote kusali ili ulimwengu mzima uweze kuheshimu na kufanya hadi ya kuweza kuisaidia Sudan ya Kusini.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 

01/08/2017 15:20