2017-08-01 13:28:00

Mito ya kujifungulia watoto yawezesha wanawake kwenda Hospital


Madaktari na  Afrika wajulikanao Cuamm watawakilisha mpango  wao uitwao mto wa kulalia  wakati wa  kujifungua katika mkutano huko Washington katika siku za hivi karibu. Hiki ni kifaa kipya ambacho kimefikiriwa kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wa Karamoja  kwenye ukanda ya Kaskazini mwa Uganda kwa kujifungua watoto katika hosptali au katika vituo vya afya. Shirika la madkatari na Afrika (Cuamm) wako kati ya washindi  wa tukio la okoa maisha wakati wa kujifungua (Saving Lives at Birth). Hii  ni changamoto kubwa ya maendeleo, ambayo imeandaliwa na Shirika la shirikisho  la Marekani USAID.

Mpango huu wa mto wa kulalia  kwa ajili ya kujifungua unataka kuonesha na kuwafundisha wanawake kwamba inawezekana kukimbilia mahali penye usalama bila kuacha tamaduni zao la muhimu ni kwenda katika maeneo yenye usalama na yenye  vifaa pia nyenzo za dharura kwa ajili yao.Matokeo haya yanatia moyo, kwasababu shukrani kwa vifaa hivi ambavyo tangu mwaka 2013 -2015 vimepata na kuongezeka kutoka idadi ya 11,242 hadi kufikia 25,592 ya wanawake walio jifungua katika maeneo yenye usalama, matokeo haya katika kanda hiyo imeongezeka kutoka asilimia 18% hadi 52%.

Mito ya kulalia wakati wa  kujifungua (Birth cusshion) inawakilisha mageuzi madogo ya kiufundi  yenye uwezo wa kukabiliana nayo hata  kiuchumi. Imewezekana  kwa mara ya kwanza na Madaktari na Afrika Cuamm mwaka 2017 huko Karamoja , mahali ambapo sasa inaonesha hatua nzuri na ongezeko katika maeneo yenye majengo ya afya  na vifaa kwa ajili ya wanawake. Ukifikiria kwamba wanawake wengi walikuwa wanapendelea kujifungulia manyumbani kwao kiutamaduni, kutokana  na kutaka wajifungue wakiwa wamelala chali.

Kwa njia hiyo kikundi cha wataalam cha madaktari na Afrika wakafikiria kutengeneza kifaa kama vile mto wa kulalia  ambapo wanawake wanaweza kutumia kwa ajili ya kujifungulia watoto kiutamaduni kama walivyozoea lakini pia akiwapo nesi  karibu wa kumsaidia. Kwa miaka minne wameweza kutawanya mito ya kulalia wakati wa kujifungua kwenye vituo  81 vya afya ukanda  mzima wa Karamoja Kaskazini mwa Uganda.
Mipango mingine  550 inayowakilisha , ina nguvu ya kuweza kusaidia hali ya afya na hasa katika uzazi  na watoto. Ikumbukwe Madkari na Afrika Cuamm ni shirika moja wapo lisilo la kiserikali kutoka nchini Italia linalojitahidi kusaidia nchi za Afrika katika vituo mbalimbali vya afya wakishirikiana pia na wauguzi wa serikali za nchi mahali walipo.Afrika kwa sasa wako katika nchi saba ambazo ni Sierra Leone, Angola, Uganda Sudan ya Kusini, Ethiopia Uganda, Tanzania, Msumbiji.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.