Wachimbaji haramu madini ni raia waovu ambao wanatishia na kuharibu nchi kwa kujiwekea
maslahi yao binafsi kwa ujumla. Hayo ni maneno ya kukemea kutoka kwa Askofu Mkuu
Gabriel Justice Yaw Anokye wa Jimbo kuu la Kumasi nchini Ghana.
Mtukio haya yajulikanayo galamsey,ni wachimbaji haramu wa madini ya dhahabu , wamekuwa
tishio linalokithiri nchini Ghana kwa namna ya pekee katika mito na hifadhi ya maji
ya taifa, ambayo yamechafuka kwasababu ya mchanganyiko wa kutumia zebaki katika kudondoa
dhahabu kutoka katika miamba inayotoa dhahabu hiyo. Askofu amesema katika kujifikiria
tu wao wenyewe bila kuzingatia taifa maana yake ni kuwa na tamaa na maovu na hivyo
inalazimu kila mmoja kufikiria kuhusu mstakabali wa nchi na vizazi vijavyo.
Kwa upande wa Askofu Mkuu anafikiria kwamba wachimbaji haramu ni zaidi wa watu waovu na pia watu wa hatari na wauaji wa wauaji wa watu bila huruma. Ni watu wasio fikiria nchi yao na watu wake.Pamoja na kwamba serikali ilianzisha kampeni ya kuzuia shughulia hizo haramu za galamsey, lakini Askofu anatoa taarifa kwamba watu hawa wanaendelea na shughuli hizo wakati wa usiku katika maeneo kama vile ya Tmso, Modaso na Diaso. Nchi ya Ghana ni ya pili katika uzalishaji wa wa dhahabu barani Afrika na ni nchi ya Kumi duniani. Pamoja na migodi ya kisheria iliyopo, lakini istoshe bado ipo nyingine ya kisirisiri. Ni vigumu kuwahesabu makundi haramu ya Galamsey ; inakadiriwa kati ya 30,000 hadi 200,000 ya watu na badhi yao ni wageni hata kutoka nchi ya China. Kumasi ni mji mkuu wa mkoa wa Ashanti ya Kusini mwa Ghana ambapo akiba ya dhahabu yote ya nchi inapatikana.
Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican
All the contents on this site are copyrighted ©. |