2017-08-01 14:32:00

Asilimia 10% ya madawa yazungukayo ulimwenguni ni bandia


Inahesabika kuwa asilimia 10% ya madawa yanayozunguka katika ulimwengu huu ni bandaia, hicho  ni kiasi yenye kuwa na  thamani ya mabilioni 85 za Euro. Taarifa hii  imetolewa na Kituo cha utafiti wa kufuatilia madawa ya bandia  mjini Paris Ufaransa . Na Kwa mujibu wa watafiti hao pia wanasema kwa upande wa Afrika chini ya Jangwa la Sahara  ni asilimia 30% ya madawa ya bandia  yanayoingia katika nchi hizo.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la kudhibiti   madawa mipakani wanasema  nchi ya India  ndiyo nchi inayo ongoza ya kwanza kutokea madawa haramu magendo na madawa yaliyofungwa vibaya  au yamekwisha muda wake. Mbele ya matukio haya  yanayozidi kuenea na ambayo nchi zinashindwa kuthibiti baadhi ya wameanza kutafuta ufumbuzi  na  kuweka katika matendo.  

Mfano mmojawapo ni JokkoSante kutoka nchi ya Senegal ambaye amezindua dhana ya kunnuua madawa  kwa njia ya mtandao, lakini njia hii bado iko katika hatua ya majaribio. Njia hii inatoa hata mfumo wa  kampuni kubwa kutoa  madawa bure kwa wale ambao hawawezi kulipia na hasa nchi ambazo kwa asilimilia 50% ya watu wake  hawana bima ya afya.
Njia nyingine pia inaitwa Sproxil ilianzishwa tangu mwaka 2009 ambayo inamsaidia mtu kuhakikisha ukweli wa dawa anayohitaji na inapotokea  kwa njia ya simu na kuhakikisha ukweli wa wa madawa hayo. Kwa miaka 6 hivi njia ya  Sproxil imehasabu sasa zaidi na milioni 50 ya ujumbe wa simu kutoka Afrika na India.

Mkutano uliofanyika nchini Liberia mwezi Aprili 2017 wa  Jumuiya ya Uchumi  wa nchi  za Afrika ya Mashariki (Cedeao) ilitangaza uzinduzi  wa kampeni ya Utafiti kuhusu magendo ya madawa na zile ambazo zimekwisha muda wake au bandia na zaidi ya hayo kampeni ya kuhamasisha. Tatizo la upatikanaji wa madawa , unaathiri hasa sehemu  kubwa ya idadi ya watu wenye hali ngumu ambao hawana uwezo wa kununua na pia  hawazingatii kutafuta chanzo cha dawa hiyo mahali inapotokea. Taarifa inaonesha pia hali hali ya kwamba , mwaka 2013 katika kutaka kupambana na malaria, dawa za bandia zilisababisha wasababiha vifo vya watoto  zaidi ya milioni 122 wa afrika.

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.