Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Baba Mtakatifu Francisko \ Hotuba

Chancellor mstaafu Kohl alikuwa ni daraja la umoja na upatanisho!

Chancellor Helmut Kohl amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 baada ya kuugua kwa muda mrefu na kwamba, anahesabiwa kuwa ni muasisi wa Ujerumani iliyoungana. - REUTERS

17/06/2017 16:33

Baba Mtakatifu Francisko amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Chancellor mstaafu Helmut Kohl wa Ujerumani aliyefariki dunia, Ijumaa tarehe 16 Juni 2017 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Baba Mtakatifu Francisko katika salam zake za rambi rambi alizomtumia Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani anasema anapenda kuungana na wote wanaomboleza kifo cha Chancellor wa umoja; kiongozi mahiri, aliyejisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wananchi wote wa Ujerumani na nchi za Ulaya. 

Baba Mtakatifu anamwombea Marehemu Chancellor mstaafu Helmut Kohl wa Ujerumani raha na mwanga wa milele umwangazie kama malipo ya jitihada zake kwa ajili ya kudumisha amani na upatanisho kati ya watu. Mwishoni, Baba Mtakatifu anatoa baraka zake za kitume kwa wote wanaoomboleza msiba huu mkubwa ndani na nje ya Ujerumani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

17/06/2017 16:33