2017-06-17 17:46:00

Askofu mkuu Nicola Girasoli ateuliwa kuwa Balozi nchini Perù


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Nicola Girasoli, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Perù. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Girasoli alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini: Trinidas, Tobago, Barbuda, Bahamas, Barbados, Dominica, Jamaica, Guyana, Grenada St. Kitts, Nevis, St. Lucia, St. Vincent Grenadine, Saints Kitts & Nevis, Suriname pamoja na kuwa ni mwakilishi wa kitume huko kwenye Visiwa vya Antille.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Nicola Girasoli alizaliwa kunako tarehe 21 Julai 1957, nchini Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapadrishwa kunako tarehe 15 Juni 1980. Kunako mwaka 2006 akateuliwa kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 11 Machi 2006 na hapo akatumwa kwenda kuwa Balozi wa Vatican nchini Malawi na Zambia. Tarehe 16 Juni 2017 ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Perù.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.