Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Tovuti ya Sinodi ya Maaskofu kwa Vijana

Tovuti kwa maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana ipo hewani - REUTERS

15/06/2017 14:52

Katika maandalizi ya ushiriki mzuri na mafanikio ya majadiliano ya changamoto na uhabarishaji wa yanayojili kuhusu maandalizi ya Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya vijana, inayoongozwa kwa kauli mbiu, Vijana, Imani na Mang’amuzi ya Miito, itakayofanyika mwezi Oktoba 2018 mjini Vatican, Sekretariat kuu ya Sinodi ya Maaskofu imefungua tovuti http//youth.synod2018.va

Hii ni fursa na mwaliko kwa vijana kushiriki kwa namna ya pekee katika maandalizi ya Sinodi hii kwa ajili yao. Katika tovuti hiyo kuna fomu za maswali dodoso zilizoandaliwa katika lugha za Kiitalia, Kiingereza, Kifaransa, Kihispania na Kireno. Fomu hizo za maswali dodoso zinapaswa zijazwe na vijana kutoka kona zote duniani kufikia Novemba 30, 2017. Iwapo vijana wengi watafanya hivyo, watakuwa wamesaidia kwa kiwango kikubwa sana maandalizi ya sinodi hiyo kwa ajili ya vijana.

Na Padre Celestine Nyanda.

Idhaa ya Kiswahili, Radio Vatican.

 

 

15/06/2017 14:52