Mitandao ya kijamii:

RSS:

Radio Vatican

Sauti ya Papa na Kanisa katika majadiliano na ulimwengu

Lugha:

Vatican \ Hotuba

Taarifa ya Fedha ya Benki ya Vatican kwa Mwaka 2016

Ukweli, uwazi, uadilifu na weledi ni kati ya mambo yanayoendelea kupewa msukumo wa pekee katika usimamiaji na matumizi ya rasilimali fedha ya Kanisa. - REUTERS

14/06/2017 09:00

Kwa miaka mitano sasa, Benki ya Vatican, IOR, imekuwa ikitoa hadharani taarifa ya mwaka ya uendeshaji wa Benki hiyo na faida inayopatikana. Taarifa hizo zimekuwa zikihakikiwa na taasisi ya kujitegemea ijulikanayo kama Deloitte & Touch S.p.A. Bodi ya Wakurugenzi Wasimamizi ya Benki ya Vatican, kwa pamoja wamepitisha taarifa ya fedha ya mwaka 2016, na wametoa pendekezo kwenye Kamati ya Makardinali Waangalizi kwamba, faida iliyopatikana kwa mwaka 2016 itolewe gawiwo kwa Vatican.

Kwa mwaka 2016, Benki ya Vatican imehudumia wateja takribani 15,00 waliowekeza mali zenye thamani kiasi cha Euro 5.7 bilioni kufikia mwisho wa mwaka, wakati kwa mwaka 2015 ziliwekezwa kiasi cha Euro 5.8 bilioni, ambapo thamani ya Euro 3.7 bilioni kati ya hizo ni Amana. Kwa mwaka 2016 zimefanyika jitihada nyingi sana katika kuboresha huduma kwa mteja, kadiri ya dhima ya Bank hiyo.

Benki ya Vatican imepunguza gharama za uendeshaji kutoka Euro 23.4 milioni kwa mwaka 2015 hadi Euro 19.1 milioni kwa mwaka 2016, kwa kurejea kwa pamoja mikataba na wadau mbali mbali wanaotoa huduma kwa Benki hiyo. Mapato ya uendeshaji kwa mwaka 2016 yamekuwa Euro 44.1 milioni, tofauti na mwaka 2015 ilikuwa Euro 45.4 milioni. Mapato makubwa yalipatikana kutokana na udhibiti mzuri wa mtaji, ambapo kumekuwa na changio la Euro 46 milioni kwa mwaka 2016. Faida kamili imekuwa Euro 36 milioni kwa mwaka 2016, tofauti na mwaka 2015 ambapo faida ilikuwa Euro 16.1 milioni. Haya mafanikio yamefikiwa kwa uwekezaji makini sana kwenye masoko ambapo hali za kisiasa zilikuwa za mashaka sehemu nyingi duniani na kushuka sana kwa faida katika biashara nyingi.

Kufikia Desemba 31, 2016 Benki ya Vatican ilikuwa imefanikiwa kutoa gawiwo la faida ya kiasi cha Euro 636.6 milioni, ambayo ni sawa na 64.5% ya uwiano wa gawiwo, ikijipambanua kwa uangalifu mkubwa na kupunguza hatari za hasara. Mbali na faida za kifedha, kumekuwa na faida za uendeshaji, mipango na utawala, mambo ambayo yalinuiwa kufikiwa katika mpango biashara wa mwaka 2016. Benki imejitahidi kuendana na taratibu mpya za AIF, zihusuzo uendeshaji wa taasisi za fedha kimataifa. Imezingatia ulipaji wa kodi, imeongeza umakini katika mifumo ya uhakiki ya ndani kwa ndani na kuboresha mifumo ya utawala na utendaji.

Na Padre Celestine Nyanda.

Idhaa ya Kiswahili, Radio Vatican.

14/06/2017 09:00