2017-06-01 16:49:00

Papa Francisko anakazia majiundo makini kwa Mapadre vijana: Sala!


Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na washiriki wa Mkutano wa mwaka  wa Baraza la Kipapa la Wakleli mjini Vatican tarehe 1 Juni 2017. Ameanza na salam na shukrani kwa shughuli zao zenye ukarimu wa kujikita katika huduma ya kikuhani mafunzo. Amemshukuru sana Kardinali Beniamino Stella Rais wa Baraza la Kipapa la Wakleli kwa utangulizi wa hotuba yake. Amesema kuwa anayo furaha kujadiliana nao juu ya tunu msingi ya utume wa kikuhani , ambapo kwa siku chache imepitishwa  misingi muhimu mipya ya kikuhani. Hati hiyo inaelezea mafunzo kamili yenye uwezo wa kuunganisha mambo yote ya maisha na kuelekezea njia ya kufundisha utume wa kimisionari. Ni njia muhimu ya wito lakini pia inayohitajika kufanyika kwa haraka.

Katika kueleza picha  hii, uzuri wa wito na uwajibu wa haraka unatakiwa, Baba Mtakatifu amefikiria kwa namna ya pekee mapadre vijana , ambao wanaishi katika furaha ya kwanza ya utume wa kikuhani lakini pamoja na kuhisi uzito uliopo. Moyo wa padre kijana Baba Mtakatifu anafafanua, unaishi kwa furaha za mwanzo lakini pia  wasiwasi wa kazi ngumu ya kitume anayojikita nayo  na wakati mwingine woga, lakini hiyo ni ishara ya hekima.
Padre kijana anahisi furaha na nguvu za mpako alio upokea, wakati huo kwenye mabega yake ananza  taratibu kuhisi uzito  wa majukumu, na kazi nyingi za kichungaji wakati huo akisubiri watu wa Mungu aliokabidhiwa.

Je ni jinsi gani huyo  padre kijana anaishi, na kitu gani ndani ya moyo wake anawaza. Je anayo mahitaji gani ili katika miguu yake inayokimbia kupeleka habari njema ya Injili , isibaki kiwete mbele ya woga na matatizo ya kwanza yanayoweza kujitokeza kwake?. Ni baadhi ya maswali ambayo Baba Mtakatifu ameuliza , lakini wakati huo akaendelea kueleza kwa kirefu zaidi. Ni lazima kukubali kwamba vijana mara nyingi wanahukumiwa kijuu juu tu na rahisi kwa kusema ni kizazi chepesi kama maji na bila kuwa na ndoto  au mawazo. Kwa hakika wapo ndiyo vijana ambao ni wadhaifu ,wenye kuwa na mwelekeo usio mzuri, wamegawanyika au kuambukizwa na tamaduni kutumia hovyo na ubinafsi. Lakini hiyo isizuie kutambua kuwa vijana wanao uwezo wa kutoa ahadi na msimamia mawazo yao juu ya maisha na kujikita katika changamoto za ukarimu. Wanao uwezo wa kutazama upeo wa maisha endelevu, wanao uwezo wa katika kulinganisha na ukosefu wa matumaini yanayokesekana katika jamii yetu.

Vijana wanao uwezo wa kujibidhisha na kubuni , ni jasiri katika mabadiliko, na hata kujitoa iwapo wanapenda kujikita kwa ajili ya wingine au kuwa na mawazo ya mshikamano, haki na amani. Pamoja na vizingiti vyao walivyo navyo,vijana ni rasilimali daima.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anatakari na kusema, tunawatazamaje makuhani wetuvijana. Je tunawacha waangazwe na Neno la Mungu ambalo linaonesha jinsi Bwana anavyo waita , anawaamini, anawatuma kwenda katika utume. Baba Mtakatifu anatazama kwa karibu wito wa Samueli kutoka katika maandiko matakatifu kwamba  wakati neno la Bwana lilikuwa bado, kwasababu watu walikuwa wamejisahau na walikuwa hawasikilizi sauti ya Bwana , ndipo Bwana alimgeukia Kijana Samueli , kijana mdogo aliyekuwa akitumikia kwenye ekalu  na akawa nabii wa watu. (1 Sam 3,1-10). Aidha Baba Mtakatifu anatoa mfano mwingine na kusema, mtazamo wa Bwana ukazidi upendo wake na kumchagua Daudi mtoto mdogo kati ya watoto wa Yese na kumpaka  mafuta akawa mfalme wa Israeli(1 Sam 16,1-13). Baadaye hata Yeremia alikuwa na wasiwasi kwamba yeye ni kijana ambaye hasingeweza kufanya utume, lakini Bwana akampa uhakika wa ubaba, akisema usiseme mimi ni kijana maana nitakuwa nawe (Yer 1,7.8).

Hata katika Injili tunaweza kusema uchaguzi wa Bwana uliwaangukia walio wadogo , na utume wa kutangaza injili ukapewa mitume wake. Hiyo kazi ya utume haitegemei na ukubwa  wa nguvu za kibinadamu, bali unatokana na utashi wa ndani na  kuancha  kuongozwa na zawadi ya Roho.
Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko anasema , hiyo ndiyo anapenda kuwaeleza mapadre vijana , kwamba wao wamechaguliwa, ni wapendwa wa Bwana, Mungu anawatazama kwa ukarimu wa kibaba , mara baada ya kumpenda kwa moyo wote , hawaachi kamwe katika hatua za safarizao. Katika macho yake wao ni muhimu na anayo matumaini kwamba wataweza kutenda utume wake aliowaitia. Aidha anaongeza ni jinsi gani ilivyo muhimu kwa padre kijana kukutana na paroko au askofu anaye mtia moyo katika mwelekeo huo, na siyo tu alikuwa akisubiriwa kwa ajili ya mahitaji au kujaza  nafasi iliyo wazi.

Kusali bila kuchoka: Baba Mtakatifu akieleza suala hili anasema, mapadre watatambua kuwa wao ni wavuvi wa watu, iwapo kwanza watajitambua kuwa nao wamevuliwa na ukarimu wa Bwana. Makuhani lazima watambue kuwa, utume wao ulinzia pale tu walipoacha ardhi yao ya kila mmoja kwa maana ya kuacha yote mipango binafsi na kutembea katika njia takatifu kwa kijikabidhi katika upendo ulio mkuu ambao uliwatafuta usiku, sauti ile ya kishindo katika mioyo yao. Kama vile wavuvi wa Galilaya , waliacha nyavu zao na kujikabidhi kwake Mwalimu. Baba Mataktifu anawambia kwamba, iwapo hawabaki wameungana naye katika sala, kuvua kwao hakutaleta mafanikio, kwa maana hiyo nawashauri wasali daima na ndiyo amri yake anawapatia.

Halikadhalika katika kueleza namna ya sala, anakumbusha kwamba miaka ya mafunzo ,muda wao wa siku ulikuwa umepangwa kiasi cha kuacha nafasi ya lazima katika sala. Lakini huo mpangilio kamili unapanza kazi za utume wa kichungahi hauwezekani kufanya. Lakini katika kukumbuka kuwa wakati wa  kipindi cha mafunzo na kuishi katika seminari walikuwa wanaishi mambo hayo katika uwiano kati ya sala, kazi na mapumziko ambayo yanawakilisha tunu msingi kwa ajili ya kukabiliana na kazi ya kitume. Kwa maana hiyo inawezekana kupanga kwa namna nyingine kwasababu , Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kuwa kila siku kuna ulazima wa kusimama, kujiweka katika kusikiliza Neno la Mungu na kuabudu mbele ya Ekaristi Takatifu. Ni muhimu kusikiliza hata mwili  ambao ni Daktari bingwa, kwani mwili unakumbusha na kuhisi  mara moja uchofu unapofanya kazi bila kuacha.

Hivyo Sala, mahusiano  na Mungu, kutunza maisha ya kiroho vinasaidia shughuli za utume , na utume kwa maana nyingine unatoa uhai wa maisha ya kiroho, na hivyo padre kwanza  anajitakafuza mwenyewe na wengine katika huduma thabiti na mazoezi ya utuma hasa kwa kuhubiri na kuadhimisha sakramenti.Ni lazima kutembea daima kwasababu padre hafiki mwisho wa safari kamwe: Anabaiki daima mtume, muhujaji katika safari ya Injili na maisha, akiwa anatazama upeo wa huduma ya Mungu katika njia ya utakatifu wa watu aliokabidhiwa naye. Mapadri wasijisikie wamefika , wala kuzimika afya kwa maana Bwana anafungua mikono yake ili kuwajazia neema . Mapadre  lazima kubaki wazi , katika matukio ya Bwana . Katika hilo ka kujifungua wazi mapade vijana wanaweza kuwa wabunifu katika utume wa unjilishaji, na daima kufanya mang’amuzi katika nafasi moja za njia ya mawasiliano , ambapo unaweza kukutana  na picha , historia, maswali ya watu, kwa kuendeleza uwezo wa kushirikishana , na mahuiano ya kutangaza imani.

Ni lazima kusali bila kuchoka, kutembea daima na kushirikishana kwa moyo maana yake kuishi maisha ya kikuhani kwa kutazama juu na kufikiria mambo makuu. Siyo kazi rahisi lakini unaweza kuwa na matumanini katika Bwana ambaye yuko mbele ya safari yetu: Na mama Maria Mtakatifu aliyesali bila kuchoka alitembea nyuma ya  mwanae na kushirikishana maisha yake hadi chini ya Msalaba aongoze na kusali kwa wajili yetu.

Sr Angela rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.