2017-06-01 16:30:00

Papa Francisko akazia umuhimu wa kudumisha tunu msingi za kifamilia


Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kuzungumza na Washiriki wa Mkutano wa Vyama vya Ulaya  vya familia Katoliki (Facce), ambao pia wanafanya maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirikisho hilo. Mkutano  wa faragha  na Baba Mtakatifu umehusu masuala ya thamani ya familia na changamoto  zinazokabiliana nazo kama shirikisho katika Bara la  Ulaya. Shirikisho la vyama  hivi ni kutoka nchi 14 za Ulaya ambao  wanayo nafasi kwenye  Baraza la umoja wa nchi za  Ulaya  kwenye mikutano ya Kimataifa vilevile wanayo katiba ya msingi wa haki katika baraza hilo.

Maadhimisho hayo na mkutano wao  mwaka kwa siku tatu umegawanyika katika sehemu tatu za tafakari ambapo pia  wameweza kuwa na fursa ya kukutana na Baba Mtakatifu tarehe 1 Juni 2017.  Shirikisho la vyama hivi katika hotuba yao, pia wameonesha shukrani  nyingi kwa Baba Mtakatifu kutokana na  Wosia wake kuhusu “Upendo wa furaha”, na Hati ya “Sifa iwe kwako”. Tarehe 31 Mei 2017 washiriki hawa wa  Shirikisho la vyama Katoliki Ulaya waliudhuria misa takatifu  na kujikabidhi katika kwake Maria ikiwa Kanisa Katoliki linaadhimisha sikukuu ya Mama Maria kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu Roma.

Naye Baba Mtakatifu katika hotuba yake ameanza na shukrani kwa familia zote zinazoundwa Shirikisho la vyama hivyo , wakiwa wakiwa katika maadhimisho ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na kumshukuru Rais wa Shirikisho hilo Bwana Antoine Renard kwa maneno ya hotuba yake aliyotoa. Miaka 20 ni michache katika kufanya kazi lakini kwa hakika ni kipindi cha kumshukuru Bwana  katika maisha na hamu kubwa ya kupeleka mbele wajibu wenu kila siku mnaojikta nao Baba Mtakatifu amesema. Hali halisi ya shirikisho kijana katika roho na katika historia, inaalikwa kuambukiza hata huduma nyingine za familia ili Ulaya iendelee kuwa  na tunu msingi wa familia. Picha ya tunundiyo ilikuwa kauli mbiu ya kuwakilisha mkutano wao wa familia mjini Roma kutoka pande za Ulaya. Baba Mtakatifu anasema. Ni mfano  ambao unatafakarisha vizuri na kushuhudiwa na wengi katika familia 

Kwa hakika familia siyo vipande vipande vya kuweka katika jumba la makubusho, kwa kwake familia inathibitisha zawadi, inajikita katika umoja au kuwa wazi katika kupokea watoto kwa ukarimu na kama ilivyo tabia ya familia inatoa  huduma za kijamii. Kwa maana hiyo familia inakuwa kama chachu inayofanya kukua ulimwengu wa kibinadamu na kindugu na ni  mahali ambapo hakuna yoyote anayejisikia kubaguliwa au kuachwa pweke.
Baba Mtakatifu anasema, shughli zao nyingi zinajieleza katika huduma kamili katika familia, ambayo ni sehemu msingi wa jamii  na ni kama walivyokubaliana hivi karibuni  viongozi wa Umoja wa Ulaya wakati wa tukio la kuadhimisha miaka 60 ya Mkataba wa Roma. Kazi  katika sekta ya Kanisa, ikiwa pia sekta ya kijamii inaweza kuonekana kwa  upesi kwamba ni kujibu mahitaji ya haraka katika mahangaiko tofauti. Lakini hali halisi kazi hiyo  inatoa jibu katika huduma ya habari njema ambayo ni familia.

Akibainisha juu ya wosia wake anasema, Baba katika Wosia wa kitume Furaha ya Upendo ndani ya familia alitaka kuonesha jinsi gani inawezakana kufanya zawadi kwa dhati ikawa njia ya nzuri na ya furaha ya upendo  wao kwa wao. Kwa mantiki hiyo, wajibu mkuu unaweza kuwa ni ule wa kuwakumbusha wote kwamba hakuna njia nzuri zaidi ya maendeleo kamili ya jamaii ambayo  inalenga kuhamasisha uwepo wa familia katika mfumo wa kijami. Hata hivyo Baba Mtakatifu anabainisha kuwa hata sasa familia inabaki kuwa msingi wa jamii na kuendelea katika ujenzi halisi kwa ajili ya wema wa watu na mahitaji ya kishirikisha kwa ajili ya maendeleo ya kudumu.Halikadhalika katika Wosia huo alitaka kuonesha jinsi gani umoja wao wa  wote ndani ya familia na juhudi za mshikamano na jamii nzima ni kwaajili ya kujikita katika wema wa wote na amani hata Ulaya.

Familia ni mahusiano ya kwanza  binafsi, ikiwa kwamba ni muungano wa watu. Muungano wa ndoa, ubaba , umama watoto na undugu vinawezesha kila mmoja kujieleza ndani ya familia ya kibinadamu. Namna ya kuishi haya mahusiano yanahitaji umoja ambao ndiyo injini ya kweli ya ubinadamu na uinjilishaji. Kwa njia hiyo leo hii hata daima inaonesha ulazima wa utamaduni wa makutano ambao unatoa thamani ya umoja dhidi ya utofauti, ushirikiswaji na  mshikamano kwa vizazi vipya. Huo ndiyo ukuu wa familia unao alikwa kujikita katika mahusiano ya kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa  Bara la Ulaya. Mtindo wa familia unaojaribu kuhamasisha siyo kitu cha itikadi za kikundi cha jamii nyingine, bali inahusiana na kutokiuka  hadhi na heshima ya binadamu. Hiyo ndiyo msingi wa heshima ambayo Ulaya inaweza hakika kuwa familia ya watu. 

Vipeo vya aina nyingi vinachanua kwa sasa katika Bara la Ulaya ikiwa ni pamoja na hali ya familia. Lakini vipeo hivyo vinachangamotisha kuweza kufanya kazi zaidi na vema kwa imani na matumaiani, Baba Mtakatifu anaeleza. Baba Mtakatifu anasema kwamba anatambua mipango yao ya kuhamasisha siasa halisi kwa ajili ya familia katika sekta ya uchumi na ajira, siyo hiyo tu bali hata inayo jikita katika kutafuta kazi yenye hadhi kwa ajili ya wote hasa vijana wengi katika kanda za Ulaya wanaoteseka na janga hili la ukosfu wa ajira.
Katika mipango hiyo na mingine zaidi inayoongozwa na sekta hiyo ya utawala, lazima iweke kipaumbele zaidi cha kuheshimu hadhi ya kila mtu. Kwa maana nyingine katokana na tamaduni ya makutano daima kuna haja  ya majadiliano ambayo ni muhimu katika kusiliza. Mazungumzo yenu daima yahusiane na matendo, ushuhuda, uzoefu na namna ya kuishi, kwamba maisha ndiyo yatoe mifano. Na ndiyo maana ya kipaumbele cha   mpango wa Mtangulizi wake Mtakatifu Yohane Paulo II aliokuwa akiiita Familia.

Aidha  amebainisha changamoto za vipeo  hivyo kwamba, vipeo vinne vinaikumba Bara la Ulaya kwa muda huu: kama vile  upungufu wa idadi ya watu, wahamiaji , ajira na elimu. Kipeo hicho lakini kinaweza kupata upeo chanya katika utamaduni wa makutano, mahali ambao wadau wa kijamii, kiuchumi na kisiasa wanaweza kuungana pamoja na kutoa majibu kulingana na kipimo cha familia, wakitambua vema kwamba familia ni rasiliamali, na ni mkataba wa mtu na mazingira yake. Kwa maana hiyo, kazi ya Shirikisho la Vyama vya Kifamilia mara nyingi wanakutana na majadiliano ya kujenga na wadau mbalimbali wa kijamii, lakini wao  bila kuficha kamwe utambulisho wao wa kikristo. Na utambulisho huo  Baba Mtakatifu anasisitiza utawafanya kutazama daima upeo wa wazi na kwa umbali. Hiyo ni kama vile wao  walivyosema katika hotuba yao kwamba utamaduni wa mbali, unawaalika katika elimu kwa ajili ya kesho. 

Ili kweza kujikita katika kazi ya familia ili isibaki katika upweke, inahitaji kujinasua katika upweke huo, inahitaji kuzungumza na kukutana na wengine, ili kutoa mahusiano katika umoja ambao yanakwenda  sambamba na maendeleo yoyote kwa manufaa ya pamoja. Baba Mtakatifu anaendelea, familia zimerithi mengi kutoka kwa mababu zao.Wao ni kumbu kumbu ya kudumu ambayo iwasukume  ili waweze kuwa na moyo wa hekima na siyo wa teknolojia ya kuunda mipango juu ya familia na kwa ajili ya familia. Wao ni kumbu kumbu; ambapo  vijana wa kizazi hiki wanalo jukumu la kutambua kwamba maisha yanaendelea mbele. Kwa mfano wa  hekima hiyo katika huduma ya utakatifu wa maisha inakamilika katika ya kizazi. Inakamilia katika kutoa huduma kwa wote, zaidi wenye kuwa na mahitaji, walemavu na yatima. Inakamilika katika mshikamano juu ya wahamiaji, inakamilika katika uvumilivi wa sanaa ya kuelimisha na kuona kwamba kila kijana anahitaji hadhi ya upendo wa familia. Inakamilika katika haki ya maisha na kupokea wale ambao hawana sauti, na inakamilika katika hali ya maisha yenye adhi kwa wazee.

Kazi ya kufanya ni kubwa na nguvu: hivyo Baba Mtakatifu anaongeza kusema, ni kwa njia ya kujibidisha katika vyama vyao , wakiwaalika familia nyingine kujiunga na kazi hiyo inaweza kuwa njia rahisi, kwasababu umoja ni nguvu. Wao wanahitaji wawe chachu inayofundisha wengine kufanya kazi pamoja wakiheshimu tofauti na hali halisi kwa ujumla.  Na mwisho amemalizia akiwatia moyo waendelee kuwa wabinifu kwa njia mpya na rasilimali ili familia ziweze kufanya zoezi  katika nyanja ya Kanisa kama vile katika jamii kwa kujikita katika aina tatu za shughuli kwa kusaidia kizazi kipya, kuwasindikiza katika kwenye hatua za maisha  ambazo mara nyingi kuna ajali za na kuwaongoza ili kuwaonesha thamani na maana ya kutembea kwa pamoja kila siku. Utume huo unaweza kuwa mchango mkubwa wa Shirikisho la Vyama Katoliki vya Familia  ameongeza, ni katika shughuli zao za kila siku kwa ajili ya familia za Ulaya. Amewabariki na kuomba sala kwa ajili yake kama kawaida.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.