2017-05-31 16:37:00

Papa: Matumaini ni kama nanga,Roho Mtakatifu ni kama tanga ya mashua!


Baba Mtakatifu Francisko kama kawaida yake, Jumatano tarehe 31 Mei 2017 ameongoza katekesi yake kuhusum matumaini ya Mkristo katika viwanja vya Mtakatifu Petro ambapo kabla ya kuanza tafakari hiyo, limesomwa somo kutoka barua ya warumi isemayo,Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. Ndugu zangu, nimehakikishwa mimi mwenyewe kwa habari zenu ya kuwa ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu ameanza na tafakri akisema; Katika ujio ulio karibu wa sikukuu ya Pentekoste hatuwezi kuacha  kugusia  mahusiano yaliyopo kati ya matumaini ya Kikristo na Roho Mtakatifu. Roho ni upepo unaotusukuma kwenda mbele na unasaidia kujisikia kuwa sisi tu wasafiri na wageni, kwani Roho hiyo  haitufanyi tuzizoee, kuwa watu wa kukaa mahali pamoja tu.

Katika Barua ya Wahebrania inafananisha matumanini kuwa kama nanga (Wab 6,18-19) katika picha hiyo, Baba Mtakatifu anasema, tunaweza kuongeza ile ya tanga ya mashua. Kwa namna hiyo, iwapo nanga inatoa uhakika na usalama wa mashua  kubaki imesisima  kati ya mawimbi ya bahari, tanga la mashua lina wezesha mwendo wa kuelea juu ya maji. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasema matumaini ni kama tanga, kwasababu tanga linakusanya upepo wa Roho , na kuufanya uwe na nguvu kam injini nayosukuma mashua kuendelea na mwendo, kwa mujibu wa mwendo kasi ikiwa katikati au karibu na ufukweni.

Mtume Paulo anamalizia barua yake kwa warumi na sikilizeni vizuri matashi yake kwamba, Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. (15,13). Baba Mtakatifu anasema tutafakari maneno hayo mazuri sana. Maelezo ya Mungu wa matumaini hayataki kuonesha kuwa  Mungu siyo tu kifaa  cha matumaini ambayo tunategemea kila siku hadi milele . Ina maana ya kusema kwamba ni Mungu yule ambaye hata sasa anatufanya tuwe na matumaini,na  zaidi anatufanya tutumaini kama yasemavyo maandiko: kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, na mkidumu siku zijazo. Hiyo ndiyo furaha ya kutumaini na siyo furaha ya kutumaini kuwa na furaha. Penye maisha leo hii kuna hata matumaini kama wasemavyo wahenga Baba Mtakatifu anakumbusha na kuongeza , ni kweli kabisa kwamba hata mahali ambapo kuna matumaini yapo maisha pia. Watu wanayo mahitahi ya matumanini ili kuishi,pia wanahitaji Roho Mtakatifu ili kutumaini.

Mtakatifu Paulo katika kuonesha jinsi gani Roho Mtakatifu anao uwezo wa kujikabidhi kabisa katika matumaini. Kujikabidhi katika matumaini maana yake kwamwe hakuna kukata  tama pia  ni kutumai kwa kila hali maana, naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, ndivyo utakavyokuwa uzao wako.(Rm 4,18). Maana yake kutumaini hata wakati inapojitokeza sababu ya  za kibinadamu za kukatisha tamaa, kama vile ilivyo mtokea Ibrahimu alipoombwa na Mungu kusadaka mwanae wa pekee Isak, zaidi kama Bikira Maria alipokuwa chini ya Msalaba wa mwanae Yesu.

Roho Mtakatifu anatuwezehsa kuwa na haya matumaini yasiyoshindwa na kutupatia ushuhuda wa ndani kama asemavyo kuwa, Roho mwenyewe ushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa warithi wa  Mungu (Rm 8,16). Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? (Rm 8,32). Matumaini hayatakabali kamwe, kwasababu  tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. (Rm 5,5).Kwa namna hiyo Baba Mtakatifu Francisko anazidi kusisitiza kwamba tumaini halitahayarishi , kwasababu Roho Mtakatifu yupo ndani anatoa msukumo wa kwenda mbele daima na ndiyo maana ya tumaini.

Kuna zaidi: Roho Mtakatifu hatufanyi tuwe na uwezo wa kutumaini peke yake bali anatufanya  tuwe wapanzi wa matumaini kama yeye anavyotoa neema kwa njia ya kutulizo, hata sisi tunaweza kuwatuliza na kuwatetea wengine. Kuweni wapanzi wa matumani  maana mkristo wakati mwingine anaweza kuwa mpanzi wa machungu na wasiwasi. Lakini njia hiyo siyo mkristo wa kweli anasisitiza Baba Mtakatifu kwamba kama wewe unafanya hivyo basi wewe siyo mkristo mwema.Mkisto  mwema anapanda matumaini daima ya mafuta ya matumaini pia manukato ya matumaini na siyo chachu inayo chakachua matumaini hayo.

Katika kuelezea vema suala hilo anatumia mfano wa mwenye heri Kardinali Newman katika hotuba yake alikuwa anawambia waamini kwamba tukijifunza kutokana na mateso yetu,  machungu yetu , na zaidi dhambi zetu wenyewe ndani ya mioyo yetu tutakuwa tumefanya uzoefu wa kazi ya upendo kwa ajili wale wenye kuwa na mahitaji. Aidha Tutakuwa na kipimo na uwezo wa kutuliza kama vile Roho  Mtakatifu anavyoshauri kwamba tunaweza kuwa  wawakili , watetezi na  kusaidia. Kwa maana hiyo maneno yetu, ushauri wetu, jinsi ya kufanya , sauti zetu ,mitazamo yetu , vitakuwa vyenye ukarimu .
Hivyo vyote vinahitajika zaidi kwa watu walio maskini,walio baguliwa , wasiopendwa, maana wote hao wanahitaji  faraja, yaani faraja na ulinzi, ambazo ni zawadi  zake  Roho Mtakatifu anazo mkirimia  kila mmoja aliyeko katika uwanja  wa Mtakatifu Petro; wote ni lazima kuwa wawakili na walinzi.

Sisi sote ni lazima kufanya hivyo kwa wahitaji, walio baguliwa, na kuhitaji msaada , wote wanao teseka zaidi. Kuwa walinzi na watoa faraja kwao. Roho Mtakatifu ni kirutubisho cha matumanini , siyo tu katika mioyo ya watu , bali hata katika kazi yote ye uumbaji. Baba Mtakatifu anasema utafikri ni jambo la kushangaza,lakini ni kweli mtume Paulo anaposema, Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, hata viingie katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu. Kwa maana twajua ya kuwa viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa. (Rm 8,20-22).
Nguvu inayofanya ulimwengu uzunguke siyo nguvu isiyojulikana na kipofu , bali ni uwepo wa Roho wa Mungu ambao unapulizia katika maji , kama yasemayo maandiko matakatifu ya kitabu cha mwanzo kwamba, “nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji” (Mw1,2).

Baba Mtakatifu Francisko amemalizia katekesi yake kwamba katika sikukuu ya Pentekoste ambayo ni sikukuu ya kuzaliwa kwa Kanisa kwamba siku hiyo itukute katika muungano wa sala na mama Maria, mama wa Yesu na mama yetu. Zawadi ya Roho Mtakatifu ituongezee wingi wa matumaini ; na zaidi tutumie matumaini hayo kwa wale wote wenye kuwa na mahitaji,waliobaguliwa.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.