2017-05-31 16:23:00

Papa amemteua Askofu mpya P. Hilary Nanman Dachelem wa Nigeria


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu wa Jimbo la Bauchi nchini Nigeria, Askofu Mteule Hilaly Nanman Dachelem, aliyekuwa Paroko na Msaidizi wa watawa wa Jimbo la Shendam nchini Nigeria.
Askofu mtule P. Hilary Nanman Dachelem, C.M.F alizaliwa tarehe 3 Juni 1966 huko Makurdi. Masomo yake ya falsafa  huko Oweri na Taalimungu  huko Enugu. Alijiunga na shirika wa wamisionari Waklaretian na kufunga nadhiri za kwanza  tarehe 8 Septemba 1988 na za milele 13 Septemba 1993. Alipata daraja la upadrisho tarehe 1 Julai 1995.

Jimbo la Bauchi liliundwa mwaka 2003 kutoka katika jimbo la Jos. Jimbo hili kuna idadi ya  wakazi 6.884.000 kati yao 80,600 ni wakatoliki. Kuna parokia 23 na kituo kimoja cha kimisionari. Mapadre wajimbo na mapadre 5 wa  mashirika , watawa 8 wakiume, watawa 8 wa kike na waseminari kuu 15. Jimbo hili limekuwa wazi tangu 21 Machi 2015 mara baada ya Askofu  Malachy John Goltok kutangulia huko kwa  Bwana Mungu.Na tangu wakati huo hadi sasa jimbo limekuwa likiongozwa na utume na Padre .P. John Keane, S.M.A. 

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.