2017-05-29 11:09:00

Wito wa Maaskofu wa Congo DRC kwa ajili ya amani katika nchi!


Maaskofu wa Jimbo la Bukavu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo  wametoa wito juu ya amani ya kudumu. Wameyasema hayo wakati wa kumalizia mkutano wao uliofanyika huko Uvira kuanzia tarehe 8-15 Mei. Katika ujumbe wa mwisho wa kazi yao,  maaskofu wanachambua hali halisi ya sasa ya maisha katika Tiafa, wakibanisha sehemu zenye mwanga na vivuli.

Maaskofu wanalaamini vitendo vile vinavyozuia amani ya nchi kutokana na mustakabali wa siasa za kitaifa. Kwa uchungu mkubwa wanakumbuka hata mateso ya utekeji nyara wa watu, ujambazi, mauaji ambayo yanakatisha tamaa na ukosefu wa  matumani kwa wakazi wa nchi. Wakati huo huo maaskofu wanasema kuwa wanao wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea kuongezeka kwa makundi ya waasi wenye silaha ambao wameleta wasiwasi mkubwa na machafuko katika maeneo mengi ya maisha ya jamii.

Ujumbe huo wa Maaskofu unaononesha kuhukumu  vitendo vya rusha ya kisiasa ambayo wameita kuwa  ni mgogogoro mkubwa wa kimaadili. Zaidi Kanisa la Congo linasikitika kuhusiana na migongano ya kisiasa ya sasa katika nchi yao ambayo wanasema kwamba inafungua milango ya vurugu na kujenga hali ya kiuchumi na kisiasa kuwa mbaya na ya kutishia maisha ya watu.  Kwa namna hiyo maaskofu wanatoa mapendekezo  ili wahusika wote wa kijamii yaani kuwa na utekelezaji wa kweli ili kwa pamoja waweze kujenga maisha yenye amani na upendo, na hiyo itawezekana tu   kutokana na juhudi za wananchi wote wenye wenye mapenzi mema kujikita katika kutekeleza wajibu huo kwa ajili ya haki ya wote.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.