2017-05-29 10:06:00

Kupaa kwa Bwana kunakumbusha uwepo wake,kuwa na Roho ya matumaini!


Katika kutafakari maana ya Sikuu ya kupaa kwa Bwana, siku 40 tangu ufufuko wake , Injili ya Mtakatifu Matayo inaelezea jinsi gani Yesu anawaaga mitume wake. Mitume walikuwa bado wanaogopa mara baada ya kupitia kipindi kigumu cha mateso ya Yesu na pia ufufuko wake. Yesu anawaachia shughuli kubwa ya kuinjilisha duniani kote ya kufundisha na kubatiza.Kwa hiyo tangu wakati ule  Kanisa linafuata utume huo.

Ni maneno ya mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya malkia wa Mbingu, wakati Kanisa Katoliki ulimwenguni, linaadhimisha sikukuu ya kupaa kwa Bwana, Jumapili 28 Mei 2017 katika viwanja vya Mtakatifu Pietro. Tangu wakati huo wa  kupaa kwa Bwana mbinguni, uwepo wa Kristo duniani umeendelea kuwapo ndani ya  mitume wake, hasa  wanao mwamini na kumtangaza. Na utume huu utadumu hadi mwisho wa historia na kila mtu, kila siku katika  uwepo wa Bwana mfufuka, ambaye anathibitisha wazi kwamba “mimi niko nanyi siku zote hadi miisho ya dunia”.  Baba Mtakatifu Francisko anasema, uwepo wa Kristo unatoa nguvu katika mateso na kitulizo wakati wa mahangaiko, kuwa  msingi wakati wa matatizo ya kitume. Sikukuu ya kupaa kwake mbinguni inatukungusha hilo.

Kupaa kwa Bwana mbinguni unatukumbusha uwepo wa Bwana na Roho ya matumaini na kuwa na uhakika wa kutoa ushuhuda wa kikristo katika ulimwengu. Kupaa kwa Bwana unatuonesha jinsi  gani Kanisa lipo, na kwamba uwepo wa Kanisa ni kwa ajili ya kutangaza Injili, vilevile furaha ya Kanisa ni kutangaza Injili. Kanisa limeundwa na watu wote waliobatizwa. Leo hii tunaalikwa kutambua vema kwamba Mungu ametupatia hadhi kubwa ya kuwajibika kwa kutangaza Injili katika ulimwengu wote na kuwawezesha binadamu wote kusogelea Injili hiyo. Hiyo ndiyo hadhi yetu na ambayo ni heshima kubwa ya kila mmoja na wabatizwa wote.

Katika kutazama juu kama Injili ilivyokuwa ikielezea mitume wake  katika sikukuu hii , Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza jinsi ya kuongeza juhudu katika hatua za utume wetu na utambuzi huo, japokuwa anabainsha kusema utume hautegemei na sisi, maana tunatambua wazi kwamba  hawali ya yote haitegemei na nguvu zetu wenyewe au uwezo wa kuandaa kama vile  kuwa na rasilimali za kibinadamu. Ni kwa njia ya nguvu ya Roho Mtakatifu tunweza kutenda utume wetu na kuwafanya wengi watambue na kufanya uzoefu wa ukarimu wa Yesu.

Sr Angela Rwezaula

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.