2017-05-27 13:38:00

Utoto Mtakatifu unahimizwa kudumisha moyo wa sala, amani na upendo


Tarehe 19 Mei 2017 ilikuwa ni kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Shirika la Kipapa la Utoto Matakatifu, au watoto wamisionari ni kama  kusema siku ya kuzaliwa kwa watoto wote wa utume wa kimisionari katoliki. Katika kufanya kumbukumbu hiyo Ubalozi  wa Robe nchini Ethiopia waliandaa sikukuu ya Utoto Mtakatifu, kwenye sherehe zao zilizofanyika  tarehe 20 Mei 2017 katika Parokia ya Adaba nchini Ethiopia. Padre Giuseppe Ghirelli mhusika wa Ofisi ya kimisionari kutoka Ubalozi wa kitume alielezea hayo katika Shirika la habari  katolii la Fides jinsi gani sherehe hiyo ilifanyika.

Padre Ghirelli anasema  sherehe hiyo iliwaunganisha maparokia ya Goba, Robe, Adaba, Herero, Dodola, Kofale, Demda  na Qarso wakiongozwa na Maparoko na makatekista wao .Walifika mamia ya watoto, japokuwa mwanzo walionekana kuwa na woga maana walijikuta katika mazingira mapya na kukutana na watoto wengine wasio wajua, lakini kama tabia za watoto walivyo haikuchukua muda mrefu kuanza kujisikia uzoefu na kujifungua kwa wengine katika michezo na nyimbo wakishirikishana wao kwa wao katika kutengeneza urafiki.

Anaendelea kusimulia,sikukuu ilianza kwa nyimbo kutoka kila kundi la parokia,na baadaye kufuatia Misa takatifu iliyoongozwa na msimamzi wa Ubalozi wa kitume  Askofu Mkuu Angelo Antolini akiwa na baadhi ya maparoko wa maparokia waliokuwako. Baada ya misa ilifuatia chakula cha mchana na pia watoto kucheza kidogo kabla ya kuanza  makutano ya maonyesho ya shughuli zao za kisanii walizo andaa kwa tukio hilo  katika maparokia yao ambapo walionesha wengine picha walizochora,nyimbo  na maigizo yanayohusu jumapili za Pasaka.

Sikukuu ilimalizika na ujumbe wa utume kwa vijana wa kimisionari, ujumbe huo umegawanyika katika majukumu manne yahusuyo sala,kushirikisha , utume wa kimisionari na ujenzi wa amani. Kabla ya kuondoka  kwao waliwakabidhi  kadi ya utambulisho wa vijana wamisionari ikiwa ishara ya kimisionari yaani  kalamu ya risasi na kwamba wakatoe ushuhuda wa kimisionari. Hata hivyo haikukosekana kutunukiwa zawadi kwa washindi wa kazi za mikono na maonyesho kutoka kila parokia ambapo nafasi ya mshindi wa kwanza walipokea watoto wa kimisionari kutoka parokia ya Robe na Goba , wa pili kutoka Parokia ya Dodola, ya tatu kutoka Adaba.

Padre Ghirelli anasema, Watoto wamerudi kwao wakiwa na majukumu ya kuwa wamisionari katika mazingira wanayoishi na kutoa ahadi ya kuweza kuwa mashuhuda wakiwasimulia wengine maana ya  umisionari wa utoto mtakatifu mara watakaporudi mashuleni kwao.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.