2017-05-27 10:50:00

Mons. Vigano aelezea maana ya Usiogope maana mimi niko nawe!


Jumapili 28 Mei 2017 ni Siku ya 51 ya Upashanaji habari ya Jamii  ulimwenguni ikiwa na  kauli mbiu “Usiogope kwakuwa mimi niko pamoja nawe (Is 43,5). kutangaza matumaini na imani katika nyakati hizi” iliyotolewa katika Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko, akiwaalika wahudumu wote wa vyombo vya habari, jumuiya nzima kuwa makini na kuhamasisha habari za kweli, kuwa na ukarimu bila kukosa matumaini ya sasa na hata ya kesho. Aidha katika ujumbe wake anasema, ni mchango ambao unatoa aina ya mawasiliano yaliyo wazi na kushirikisha daima ambapo anawataka  kamwe wasiruhusu ubaya au nafasi ya upendeleo,bali kujikita katika kutafuta kuweka mwanga zaidi na uwezekano wa kutafuta ufumbuzi. Kadhalika kuwa na msukumo wa kutafuta mbinu makini na kuwajibika kwa watu hasa watendaji wa mawasiliano  wanaotoa  habari hizo. Katika Ujumbe huo Baba Mtakatifu Francisko anawaalika kila mtu, wake kwa waume wa  nyakati za sasa kutoa simulizi zenye mantiki ya habari njema na ndiyo  matarajio daima hata katika sinema nzuri.

Kwa njia hiyo, Monsinyo Dario Vigano  Mwenyekiti wa Sektretarieti ya Mawasiliano mjini Vatican  akihojiwa na wandishi wa habari mapema wiki hii alipata ya kusema  akiwa Mjini Cannes katika kuwasilisha picha ya Baba Mtakatifu Francisko itakayotolewa hivi karibuni yenye kuwa na kichwa cha maelezo “Papa Francisko mtu wa neno”. Monsinyo Vigano anaelezea  kuhusu  ujumbe wa  tukio la  Siku ya Mawasiliano  Kijamii ulimwenguni  kwamba, yeye anawaalika watu wasimulie historia zilizo na vivuli na mwanga, dhambi na neema  kuanzia katika mtazamo wa akili na kiroho, muhusika au mtazamaji katika upeo, bila kukataa  matukio ya sasa lakini wakati huo kutambua namna ya kutafuta ufumbuzi au ubunifu na zaidi  njia muhimu za kuleta matumaini.Kwa njia ya Sinema Baba Mtakatifu anataka kupitia njia hiyo ili kuwafikia jumuiya nzima inayoundwa na wake kwa waume kila imani, itikadi  na tamaduni, aidha wenye kuwa na shahuku ya kijibu maswali yao.

Kwa kufuata ujumbe wake Baba Mtakatifu wenye kauli mbiu “usiogope maana mimi niko pamoja nawe  kutangaza matumanini na imani katika nyakati zetu”,  Monsinyo Vigano anasema; jambo jingine muhimu zaidi ni kutazama kauli mbiu hiyo kwa kina kuanzia mwanzo wake kwa maana wengi wanaweza kuchukulia sehemu ya pili yaani kutangaza matumaini na imani katika nyakati hizi, badala yake kwanza  lazima  kutazama nabii Isaya asemaye usiogope maana mimi niko nawe,( Is 43,5) maneno haya lazima yatazamwe kwa kina bila kuyaweka pembeni maana nabii Isaya anatoa ujumbe wa kitulizo kutoka kwa Mungu kwa watu wake. Hii ni kama kusema anaongeza Monsinyo Vigano kwamba, fungulia mioyo utulivu wa uwepo wa Mungu kwa njia hiyo mawasiliano yenu yatapata njia ya matumaini na kuaminiwa.

Watu wenye mioyo migumu ambayo maandishi matakatifu yanaeleza kuwa,  watu hao walikwenda mbali na Mungu, lakini njia hiyo iliwafanya wawe na wasiwasi na kujisikia yatima, kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko; watu hao wanahitaji kusikia kwa upya ukaribu wa Mungu katika maisha yao; kwa njia hiyo wanaweza kwa wapya kuendele na safari yao na kurudia njia ya uaminifu wa Agano. Kwa maana hiyo hata mawasiliano yamekuwa daima na matukio ya vurugu na giza, hasa katika kutafuta uwezekano wa mara kwa mara kuonekana au kutafuta kujulikana badala ya kutafuta umuhimu, Monsinyo anabainisha kusema, sasa mawasiliano hayo  yanahitaji kupata utulivu. Anaendelea kusema,  Mawasiliano siyo tu sehemu ya uwezekano wa dhambi kwa mfano  kufikiria tu mashtaka, uvumi, majanga, lakini pia ni sehemu ya ukaribu na huruma, kwa njia hiyo ndiyo maana maandishi matakatiu ya Nabii Isaya anasema; basi usiogope kwa maana mimi ni  pamoja nawe.

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa hakika anatoa tahadhali ya kuwa makini kwa maana siyo kusema ni mantiki ya wema , ni kuhusu kukuza habari njema mbele ya upotofu wa habari, mahali ambapo itatokea kupuuza mateso au kuangukia ndani ya woga ambao hauleti matumaini au kuguswa kwasababu ya kashifa za uovu. Kwa njia hiyo ni lazima  kutatufa uwazi na ubunifu wa mawasiliano katika mtindo ambao kamwe uko tayari kutoa nafasi njema na zinazopinga kuumiza. Hiyo inawezakana kwasabu ya kujaribu kutafuta mtindo wa mawasiliano ulio wazi  au kuangukia katika majaribu ya kutafuta makuu, lakini kujaribu kutoa mwanga na uwezekano wa ufumbuzi zikihamasha mbinu makini na kuwajibika kwa ajili ya watu ambao habari hiyo inawasilishwa. Hiyo siyo kunyume na mantiki ya habari mbaya inahitaji kutoa kwa nguvu zote mantiki yenye ishara ya habari njema ambayo ni habari halisi.

Hata hivyo Baba Mtakatifu katika ujumbe wake anatoa mwaliko wa kuelezea habari wa mwanga na kivuli, bila dhambi na neema, na daima kusonga mbele kwa  akili na moyo wa msomaji au mtazamaji kwa upeo wa macho kwamba, bila kukanusha matukio halisi yalivyo, lakini wakti huo huo ni kutambua jinsi gani ya kuondokana angalu au uwezekani wa matumaini. Monsinyo Vigano aidha anasema ; hotuba za Baba Mtakatifu daima zinawasilisha ujumbe rahisi na kwa upande mwingine  ni kama asemavyo kwamba kila aina ya mawasiliano yana mzizi  katika utashi na katika utashi wa kuwasilisha kusimulia hali halisi kwa njia ya furaha ya Injili. Kwa maana hiyo picha ugeuka kuwa jambo jema zaidi linalo wakilisha ujumbe wenyewe.

Ujumbe wake Baba Mtakatifu Francisko anatumia neno la matumaini hivyo Monsinyo Vigano  anasema kwamba, ukitazama katika katekesi zake za kila jumatano, zinaelezea kwa kina zaidi hatua muhimu za matumaini ya kikristo. Akikumbuka meneno aliyosema tarehe 7 Desemba 2016 kwamba, matuamaini ya Mkristo ni muhimu kabisa  kwa sababu tumaini halitahayarishi. Matumaini ya tamaa ndiyo na  hivyo tuna haja sana, hasa wakati huu ambapo giza nene linazidi kutanda na wakati mwingine unaweza kuahisi kwamba ni kupotea mbele ya maovu na vurugu zinazotuzunguka na mbele ya machungu ya ndugu zetu.Inahitaji matumaini! 

Sr Angela Rwezaula 
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.

 








All the contents on this site are copyrighted ©.