2017-05-25 12:10:00

Viongozi nchini Sudan Kusini wasaidie harakati za kibinadamu!


Pande zote zinazopigana ni lazima kusitisha vurugu na kushirikiana kwa pamoja katika kazi ili kuhakikisha kwamba chakula na msaada  unafika   kukidhi haja ya  idadi ya watu na mwisho kukomesha njaa inayokithiri. Huu ni ujumbe ulitolewa Jumatano tarehe  24 Mei 2017 na Mkurugenzi wa FAO José Graziano da Silva pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, David Beasley wakati wa  ziara yao katika  mojawapo na maeneo  yaa walioathirika na mgogoro wa chakula  nchi ya Sudan ya Kusini.

Ni karibia milioni 5.5 za watu katika nchi ambapo nusu yao wanateseka na njaa ya kutisha, hawajuhi mlo wao utafika lini wakati huo kiangazi kinakaribia mwezi wa saba. Zaidi ya watu 90,000 wamekumbwa na ukame ambao baadhi ya maeneo ya nchi walikwisha tangaza kipeo cha ukame na njaa nchini . Katika hali hii Bwana Graziano da Silva e Beasley wanasisitiza umuhimu wa jibu la haraka  ili kuongeza nguvu za kibinadamu kuwasaidia wakulima na katika kuvua samaki.Wanasema ni lazima kuokoa maisha ya watu sasa kabla hali haijawa mbaya zaidi na kupunguza hatari ya vifo na gharama. Lakini yote hayo  iwapo vurugu zingeweza kusitishwa kwasababu ndiyo yanafanya kudorora kwa hali ya kibinadamu katika kutoa huduma hiyo.

Bwana da Silva anasema ”hali ni mbaya lakini hatujachelewa katika kuokoa maisha ya watu .Tunaweza bado kuzuia maafa yasizidi kuwa makubwa japokuwa kuna vurugu zinazoendelea."Katika hali hii haiwezekani kuwapo maendeleo bila kuwa na amani .Watu lazima wapate chakula na wazalendo wanapaswa wafanye  kazi katika mashamba yao na katika kuchunga mifugo yao”. Anasema Bwana da Silva.
Aidha Bwana Beasley baada ya kuona mazingira wanayoishi watu hao amesema, ”lazima watu wawe na chakula, matibabu kwa ajili ya watoto wenye utapia mlo,kusaidia watu wanaotaka kuvua samaki na kulima bustani ndiyo vitu muhimu vya kuwasaidia watu wanaopambana kati ya maisha na kifo”. Lakini hiyo haitawezekana kuendelea kulazimisha nguvu za msaada kutoka nje; kwasababu kwanza vurugu  zikomeshwe  ili kuwekeza mambo muhimu kwa ajili ya watoto wa Sudan ya Kusini na kuwapa matumaini endelevu wanayostahili.

FAO na WFP wanakabiliana ukosefu wa dola za kimarekani  milioni 182 kwenye miezi 6, pamoja na hayo bado wana matatizo ya ukusanyaji wa misaada mbele ya mahitaji yanayozidi kuongezeka katika  kipeo kinachoikumba dunia. Hayo yamesema na Bwana Beasley wa  WFP kwamba wafadhili wamesaidia Sudan ya Kusini kwa miaka mingi, lakini pia WFP wataendelea kuwa karibu na watu wa Sudan ya Kusini katika mahitaji yao pamoja na Kipeo kinachokabili  dunia nzima ambayo pia wanahitaji msaada wa haraka.Lakini pamoja na hayo yote anabainisha kiongozi huyo kwamba msaada wa Sudan ya Kusini utawezekana, iwapo pia  viongozi wa nchi wataonesha mapenzi mema katika kusaidia harakati za juhudi za kibinadamu kwa kuondoa ushuru usio na maana unaosababisha kuchalewesha  au kuzuia mchakato wa msaada wa kibinadamu kuingia katika nchi hiyo  kuwawasaida watu wao.

Aidha anasema , WFP inalenga kusaidia angalau watu milioni 4.1 mwaka huu katika Sudan Kusini, kwa  kutoa chakula kwa idadi ya watu katika maeneo ya mbali vinginevyo hawatakuwa na  kitu chakula  kwasababu wametengwa kutokana na  mapigano. WFP pia inasambaza matibabu maalum ambayo husaidia mama na watoto kupambana na utapiamlo na hutoa msaada wa kifedha  ili kuruhusu wale  waathirika zaidi waweze kununua chakula katika maeneo ambayo chakula kinapatikana japokuwa upatikanaji ni bei kubwa.

Hadi sasa watu milioni 2.9 wamefaidika na FAO  kukidhi  maisha yao  wakati wa kiangazi kwa sasa; FAO pia wanasambaza mbegu na kuandaa maonyesho ya mbegu ili kusaidia watu milioni 2.1 mwishoni mwa msimu mkuu wa kilimo . Hadi sasa takriban watu 200,000 wamepokea vifaa na mbegu za mboga na nyavu za uvuvi katika maeneo yote ambayo yalitangazwa kuwa na kipeo cha kitaifa.
Kampeni ya chanjo iliyofadhiliwa na FAO imewezesha kutibu milioni 1.8 ya watu  kutoka mwanzo wa mwaka na lengo lake ni kufikia milioni 6 kufikia mwisho wa mwaka huu. FAO pia wanazidi  kusambaza nyavu za uvuvi katika maeneo ya walioathirika na njaa, ambapo wanaishi katika mabonde na kuwa na uhaba mkubwa wa vyanzo vya chakula.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.