2017-05-25 14:19:00

AF.Kusini:Askofu alaani vitendo vya kihalifu dhidi wanawake na watoto


Kila uhalifu dhidi ya wanawake na watoto husababisha maafa ya jamii .Ni malalamiko ya Askofu Mkuu Stephen Brislin wa jimbo Kuu la Cape Town na Rais wa Baraza la Maaskofu Afrika ya Kusini (Sacbc) katika ujumbe ambao analaani vikali  vitendo vya unyanyasaji unaofanywana dhidi ya wanawaka na watoto nchini humo. Askofu Mkuu anasema wakati wahika wa matendo hayo wamewekwa mbaroni na kuendelea na michakato mahakamani, waathirika wanakabiliwa na matatizo makubwa wakati wa mchakato huo kwasababu ya gharama za binadamu na kijamii kwani  ni kubwa mno.

Rais wa Baraza la Maaskofu wa Afrika anaonesha takwimu za utafiti wa hivi karibuni  uliofanyika nchini Afrika ya Kusini kwamba, mtoto mmoja kati ya watano ameathirika na vitendo vya kijinsia, wakati asilimia 75% ya watoto wanakabiliwa na uonevu mashuleni na majumbani. Wimbi la unyanyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto hivi karibuni unatoa mshituo mkubwa kwa nchi. Anaongeza kusema, kitu cha kushangaza zaidi ni kwamba waathirika wengi wanawafahamu wahusika wa matendo haya, hivyo  kiukweli ni jambo linalofufua maswali ya kujiuliza badala ya kupata jibu, anasema Askofu Mkuu Brislin.

Pamoja na unyanyasaji huo  ndani ya familia, mashule na katika jamii unao kithiri,anaongeza kusema kuwa, kuna vitendo vya ulivi wa pombe na madawa ya kulevya. Zaidi ya waathirika ni vijana ambao wanaunganika katika magenge. Kitendo cha kushiriki katika genge anaongeza kusema, limekuwa ni tukio la kawaida ambalo baadaye linageuka kuleta  vurugu au genge la ubakaji. Hata hivyo suluhisho siyo tu uwepo wa polisi au kuwapeleka gerezani vijana hawa bali, anasema Askofu Mkuu ni lazima kutafuta mbinu ya kuweza kuwasaidia vijana hasa katika kuwashirikisha kweli kuna nia ya kutaka kupunguza vurugu hizi.

Halikadhalika Askofu Mkuu anasema kwamba, badala ya kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha katika mifumo ya makosa ya jinai na  majengo ya magereza ni wito kwa waamni wote wa Kanisa katoliki na jamii kuongeza michango yao ya fedha kwa ajili ya mipango  ya kuwasaidia wazazi. Kwa maana ya kwamba kuna haja kubwa ya kupamna na kukomesha hali ya kutokujali matendo ya vurugu na unyanyasaji ndani ya familia, mashuleni, Kanisani na katika jamii kwa ujumla.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.