2017-05-24 08:53:00

Maaskofu wapendekeza majina ya Rais wa CEI!


Baraza la Maaskofu Katoliki Italia katika mkutano wake wa 70 uliofunguliwa kwa hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 22 Mei na unatarajiwa kufungwa rasmi Alhamisi, tarehe 25 Mei 2017 umehitimisha agenda ya uchaguzi mkuu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia baada ya Kardinali Angelo Bagnasco kung’atuka kutoka madarakani. Maaskofu waliopendekezwa kwa Baba Mtakatifu Francisko ambaye atamteua mmoja kati yao ni: Kardinali Gualtiero Bassetti, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Perugia. Wengine ni Askofu Franco Giulio Brambilla wa Jimbo Katoliki la Novara na mwishoni ni Kardinali Francesco Montenegro, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Agrigento. Majina haya tayari yamekwisha wasilishwa kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya utekelezaji zaidi!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.

Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican.








All the contents on this site are copyrighted ©.