2017-05-23 14:12:00

Maisha ya Makardinali watano wapya waliotangazwa na Papa!


Jumapili tarehe 21 Mei 2017 wakati wa sala ya Malkia wa Mbingu Baba Mtakatifu Francisko aliwatangaza maaskofu wakuu wapya  watano  kutoka sehemu mbalimbali za dunia kuwa makardinali wapya kushiriki Mkutano wa Baraza la Makardinali tarehe 28 Juni 2017, wakati huo huo kuwekwa wakfu makardinali hao tarehe 29 Juni katika sikukuu ya watakatifu Petro na Paulo.
Makardinali wapya ni Askofu Mkuu Jean-Zerbo wa Jimbo Kuu la Mali aliyezaliwa Sgou tarehe 27 Desemba 1943 na kupata mafunzo ya juu huko Lione Ufaransa.  Alipata daraja la upadre tarehe 10 Julai 1971 huko Segou. Shahada ya masomo ya Biblia Roma na kuendelea na masomo ya Maandiko Matakatifu 1977-1981. Tangu mwaka 1982 na kuendelea  alifanya utume kama Paroko wa Markala na kuwa Profesa katika Seminari Kuu ya Bamako. Aliteuliwa kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Bamako tarehe 21 Juni 1988 na tarehe 19 Desemba 1994 akahamishwa kuwa Askofu wa Jimbo la Mopti. Tarehe 27 Juni 1998 akateuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Bamako. Katika nchi yake amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha mchakato mzima wa amani nchini Mali. Amejihusisha sana katika mapambano dhidi ya ubaguzi na kusaidia kuhamasisha mapatano na mshikamano kati ya watu wa Mali.

Askofu Mkuu Juan José Omella  wa Jimbo Kuu la  Barcelona nchini Uhispania, alizaliwa tarehe 21 Aprili 1946 huko Cretas. Alimaliza masomo yake ya falsafa na teolojia katika Seminari ya Saragozza na pia katika Kituo cha mafunzo ya Mapadri wa Shirika la Yesu(Mapadre weupe) huko Lavonio na Yerusalem. Alipata daraja la upadre tarehe 20 Septemba 1970. Katika utume wake wa kikuhani aliwahi kuwa paroko msaidizi na baadaye kuwa paroko mwaka 1990 na mwaka 1996 akawa msaidizi wa Askofu katika Jimbo la Saragozza. Ameliwahi kufanya umisionari kwa mwaka mmoja katika nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wakati ule ikiitwa Zaire. Tarehe 15 Julai 1996 alichaguliwa kuwa Askofu msaidizi wa Saragozza, tarehe 27 Oktoba 19 Decemba 2003 aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Kitume huko Huesca .

Tangu tarehe 19 Oktoba 2001 hadi 19 Desemba 2003 akawa mwakilishi wa kitume huko Jaca. Tarehe 8 Aprili 2004 akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo la Calahorra na La Calzada-Logrorio. Tarehe 6 Novemba 2014 akatangazwa kuwa mmoja wa Baraza  la kipapa la Maaskofu. Tarehe 26 Desemba 2015 akatangazwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Barcellona. Amewahi kushika nafasi ya Kamati ya Baraza la Maaskofu kwa ajili ya uchungaji kijamii hadi mwaka 1996 na kama Rais  mwaka 2002-2008 na akachaguliwa tena kwa miaka mingine mitatu kuanzia 2014-2017. Amewahi kuwa mwakilishi  wa kamati ya Baraza la maaskofu kichungaji  (1996-1999) na utume wa walei mwaka  (1999-2002 / 2008-2011). Katika Baraza la Maaskofu wa Ulaya kwasasa yeye ni  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji tangu  tarehe 14 Machi 2017.

Askofu Mkuu  Anders Arborelius, (ocd) wa Jimbo Kuu la Stokholm nchini Sweden alizaliwa huko Sorengo tarehe 24 Septemba 1949. Alibadilisha dhehebu kuwa mkatoliki akiwa na miaka 20. Mwaka 1971 aliingia katika Shirika  la Mapadri Wakalmeli  huko  Norraby mahali ambapo baada ya mafunzo ya utawa alifunga nadhiri za milele huko Bruges nchini Ubelgiji mwaka 1977. Alimaliza mafunzo yake ya  kimajiundo ya kifalsafa na Teolojia nchini Ubelgiji na Tresianum Roma. Wakati huo huo alifanya mafunzo  ya lugha za kisasa katika Chuo Kikuu cha  Lund. Tarehe 8 Septemba 1979 allipata daraja la Upadre  huko Malmö. Tarehe 29 Desemba 1998 alichaguliwa kuwa Askofu, Kanisa Kuu Katoliki la Stokholm .Na kuwa Askofu wa Kwanza mkatoliki katika nchi ya Sweden na mzawa wa sweden tangu wakati  wa mageuzi ya kiluteri ya mwaka 1500.
Tangu 2005 hadi 2015 amekuwa Rai wa Baraza la maaskofu wa  Scandinavia , wakati huo huo mwaka 2015 akachaguliwa tena  Msaidizi wa Baraza hilo. Alitangazwa kuwa mwakilishi wa Kamati ya Baraza la Kipapa kwa Familia tangu 2002 hadi 2009 na tarehe 21 Januari 2014 mwakilishi wa Baraza la kipapa la Walei.

Askofu  Mkuu  Louis-Marie Ling Mangkhanekhoun alizaliwa tarehe 8 Aprili 1944 huko Laos. Majiundo yake ya kitaaluma alifanyia huko Laos na Canada. Alipata daraja la upadre terehe 5 Novemba 1972 na kuwa msaidizi wa Kitume wa Vantiane. Anaongea lugha ya khumu , laotioano, kifaransa na kingereza. Amewahi kuwafudisha  makatekista na kutembelea vijiji vingi vilivyoko kwenye milima. Tangu 1975 alichaguliwa kuwa paroko na msaidizi wa Kitume wa Vientiane. Tarehe 30 Oktoba 2000 alitangazwa kuwa Msaidizi wa Kitume wa Pakse na kuwekwa wakfu wa Kiaskofu tarehe 22 Aprili 2001. Alitangazwa kuwa Balozi wa Kutume katika makao ya kitume ya Vientiane tarehe 2 Oktoba 2017. 

Askofu Mkuu Gregorio Rosa Chávez, Msaidizi wa Jimbo Kuu la San Salvador - El Salvador, alizaliwa huko  Sociedad  tarehe 3 Septemba  1942. Majiundo yake katika Chuo Kikuu Katoliki cha Lovanio, nchini Ubelgiji  mwaka  (1973-1976), na kupata shahada ya Mawasilano ya jamii. Anaongea lugha ya kifaransa , kingereza , kireno na kiitaliano. Mwaka 1965 alihudumia katika seminari ndogo ya Jimbo  la Mtakatifu Miguel. Alipata daraja la upadre terehe 24 Januari 190 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Miguel huko Salvador katika mikono ya Askofu  José Eduardo Alvarez Ramírez, alishika nafasi  ya ukatibu  wa jimbo la Mtakatifu Miguel  mwaka (1970 - 1973); Nafsi nyingine ya utume kama Paroko wa Kanisa la Rosari kwenye mji wa Mtakatifu Miguel tangu 1971-1973; Mkurugenzi wa mawasiliano Jimbo, Radio Paz, na Padre mlezi wa wa Seminari ya Chaparrastique dal 1971-1973; ameshika nafasi ya kuwa padri wa kiroho katika mashirika na vyama mbalimbali vya utume wa walei (1970-1973); Gombera wa Seminari ya Kati huko Mantaria ya Mtakatifu Yosefu ,na  Mtakatifu Salvador (1977-1982); Profesa wa Taalimungu katika Seminari ya Mtakatifu Jose Montafia (1977-1982); ameshiriki katika Baraza la Mipango ya Seminari za Amerika ya Kusini (1979-1982). Alitangazwa kuwa Askofu msiidizi wa Jimbo  Kuu la Mtakatifu Salvador, tarehe  3 Julai  1982. Kwa sasa alikuwa ni Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Francisko huko  na Rais wa Caritas kwa ajili ya Amerika ya Kusini, Visiwa vya Karibi na Caritas ya taifa.

Ikumbukwe  Ibada ya Misa Takatifu  katika sikukuu ya Mtakatifu Petro na Paulo inayoadhimishwa na Kanisa Mama Katoliki kila tarehe 29 Juni ya kila mwaka na kwa namna ya pekee mjini Vatican kuna utamaduni wa mapokeo ambao Baba Mtakatifu hubariki Pallio takatifu za kuvishwa makardinali wapya, zamani walikuwa wakivalishwa na Baba Mtakatifu mwenyewe, lakini kwa miaka ya hivi karibuni zoezi hili limebadilishwa kwani Pallio hizo za kuvishwa Maaskofu wakuu wapya , zinafanyika kwenye majimbo yao Makuu na Mabalozi wa Vatican katika nchi mahalia.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.