2017-05-22 16:04:00

Mali: Askofu Zerbo amestaajabu kutangazwa kuwa Kardinali mpya!


Askofu Mkuu wa Mali ameshangazwa na habari, kwasababu hakuwa anatambua kutangazwa kuwa Kardinali. Ni Habari kutoka katika Shirika la Habari Katoliki la  Fides, kupitia kwa Padre Dembele Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Mali akieleza jinsi gani nchi hiyo wamepokea tangazo  kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko ambaye Jumapili 21 Mei 2017 Baada ya kumaliza sala ya Malkia wa mbingu alitangaza kushiriki kwa makardinali watano wapya katika Mkutano wa Baraza la makardinali tarehe 28 Juni 2017 kati yao akiwemo Askofu Mkuu  Jean Zerbo wa Jimbo Kuu ka Bamako. 

Habari hiyo imepokelewa kwa shangwe kubwa katika  nchi. Hata Rais wa Nchi ya Mali Ibrahim Boubacar Keïta alimtumia ujumbe wa kumpongeza Askofu Mkuu pia  kumshukuru hata Baba Mtakatifu Francisko:Aidha  maaskofu wa Mali pamoja na waamini wote Katoliki wanayo furaha kubwa ya habari hiyo. Kwa namna ya pekee jumuiya ya Bamako ilijionesha furaha  na shangwe kubwa kwa nyimbo na makofi mara baada ya kupokea taarifa hizo.Aanaongeza kusema kuwa habari hiyo imeleta furaha siyo tu kwa upande wa wakatoliki bali hata nchi nzima ya Mali ambayo imepokea vema tangazo hilo.
Padre Dembele anaeleza ya kwamba, watu wa Mali wamepokea  kwa furaha kubwa ya kutangazwa Askofu Mkuu Zerbo kuwa Kardinali  kwenye ujumbe wa  wa Baba Mtakatifu ambao kwa hakika unajieleza hawali ya yote katika Kanisa mahalia. Ni utume ulioanza muda mrefu na zaidi unaondeleza  juhudi za upatanisho wa nchi. Hata hivyo ni wito kwa watu wote wa Mali ili waweze kuondokana na kipeo kilichoanza tangu mwaka 2012 ili wapate  kutembea katika nchi ya mapatano na amani.

Aidha kipeo cha 2012 kimeonekana katika nchi ya Mali Kaskazini kutokana na kuzuka  kwa makundi ya kijihadi .Hata hivyo uwepo wa Manajeshi wa Ufaransa  wakifuatia Kikosii cha utume wa Umoja wa mataifa cha kulinda amani  waliweza kukomboa maeneo yaliyokuwa yamevamiwa. Pamoja na hayo Padre Dembele anasisitiza kwamba nchi ya Mali  inapaswa kukabiliana sasa na vurugu zinazojitokeza  hapa na pale, ambazo zinasababishwa na mashambuliz iya makundi yenye silaha dhidi ya maeneo ya Kaskazini na ya kati ya nchi ambayo yanaonesha kuwa usalama wa nguvu.

Sr Angela Rwezaula
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

 








All the contents on this site are copyrighted ©.